Na Renatha Kipaka, Bukoba
Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba WilÂaya Muleba mkoani Kagera​ wametakiwa kuÂfanya vyema katika utekelezaji wa​ majukÂumu yao usimamizi wa rasÂlimali ardhi utakao saidia kupunguza​ keÂsi zinazokatiwa rufaa ya mahakama kuu.
Hayo yameelezwa jana Juni 21, 2021 na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu​ Kanda ya Bukoba​ Dk. Ntemi Kilekamajenga wakaÂti wa kuapisha wajumÂbe wateule​ wanne wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilayani humo.
Jaji Kilekamajenga amesema, kesi zinazofÂikishwa mahakama kuu kutoka kwenye mabarÂaza ya ardhi wilayani asilimia kubwa​ ziÂnahushisha migogoro ya ardhi
“Tuwakateni tu mwenÂde kwenye majukumu yenu kusimamia hizi kesi za ardhi ambazo katika mahakama kuu hapa, kesi nyingi asÂilimia kubwa ni masuÂala ya ardhi migogoro punguzeni hiyo hali huko kwenye Baraza yenu,” amesema KilekÂamajenga.
Amesema kiapo walichÂotamka wajumbe hao kinapaswa kuangalia zaidi katika haki na jinsi ya kusaidia watu wenye uhitaji wa utatuzi kwÂenye migogoro ambayo ushiriki wa maamuzi unahusisha baraza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamzora amesema shughuli ya ardÂhi sio migogoro pekee bali kuongeza hamaÂsa kuanzisha kipato cha uchumi.
Alisema, mkoa huo unakaliwa na wakazi wapatao700,000 ambao wanaweza kufanÂya ongezeko la uchumi kuongezeka endapo migogoro ya ardhi​ ikiondolewa.
“Ngoja niwaeleze, watu ndiyo wanaoongezeka​ na sio ardhi mkisimÂamia vizuri nafasi zetu tutaondoa migogoÂro katika huu mkoa na kuzalisha kwa lengo kukuza la uchumi,” amesema Prof. KamÂzora.
Awali, Kaimu Mkuu wa kitengo cha Sheria, oÂfisi ya mkuu wa mkoa, Job Mrema alÂitaja majina ya wajuÂmbe hao Justus MtaleÂmwa, Batolomayo LugaiÂmukamu, Pastory IhumbÂika, Georgia Machumu.