Kihongosi Katibu Mkuu mpya UVCCM

0
483

Na Ramadhani Hassan, Dodoma

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Kenan Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mpainduzi (UVCCM).

Uteuzi huo umekuja kufuatia aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, Raymond Mangwala kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Juni 19, mwaka huu.

Akitangaza leo Jumanne Juni 22,2021, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu iliketi leo chini ya Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan.

Amesema Kihongosi ni kiongozi mwenye uzoefu kwani ameanzia ngazi za chini kuanzia Uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa na pia mkimbiza Mwenge wa Uhuru.

Aidha, kuhusu nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM, Shaka amesema kuwa uamuzi wake bado.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here