27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito waiangukia Serikali

NA ELIUD NGONDO, MBARALI

WANAWAKE wa Kijiji cha Mkandami wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wameiomba Serikali ya kuwapatia jokofu la tiba kwa ajili ya kina wajawazito ili kuepukana na kutembea umbali wa kilomita 28 kufuata huduma.

Kauli hiyo, imetolewa mwishoni mwa wiki na Diwani wa Kata ya  Mwindi, Yusuph Mhando (Chadema) wakati wa kikao cha baraza la madiwani.

Alisema wajawazito, wamekuwa wakiteseka kutembea umbali mrefu kutokana na kukosa kifaa hicho.

Alisema wananchi walijitolea kujenga na kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati ya Kijiji cha Mkandami na kuanza kufanya kazi, lakini kumekuwapo changamoto.

Alisema kutokana na wajawazito kutembea umbali mrefu, kuna baadhi wamekuwa wakipatwa na madhara mbalimbali na kusababisha mimba kuharibika.

Alisema wameshuhudia baadhi ya wajawazito wakijifungulia njiani, watoto kupoteza maisha na hata  mama zao.

“Kutokana na wajawazito kutembea umbali mrefu wa kilomita 28 kufuata huduma ya kriniki na chanjo katika kituo cha afya cha Mawindi, tumeshuhudia baadhi yao wakijifungua watoto njiani na wengine wakipoteza maisha,” alisema Mhando.

Naye Diwani Viti Maalumu, Salome Stemile (CCM), alisema kitendo cha kutembea umbali mrefu, Serikali inatakiwa kusikia kilio hicho.

Alisema mjamzito, anatakiwa apate huduma hizo zikiwa karibu naye.

Aidha akitoa ufafanuzi wa suala hil,o Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Godfrey Mwakalila alisema tayari wanategemea kupata majokofu 18 ambayo yatasaidia  kuepukana na changamoto hiyo.

Alisema Jokofu mmoja, linagharimu Sh milioni 58 hivyo waliwaomba kupitia taasisi za kiraia ili kutatua changamoto hiyo.

mwisho

Anayedaiwa kuvunjwa mgongo kuanza tiba leo

Na Elizabeth Kilindi,Njombe.

HOSPITALI ya Utengamavu INUKA iliyopo wilayani Wanging’ombe mkoa Njombe, imesema kuanzia leo itaanza kutoa tiba kwa mwanafunzi Hosea Manga ambaye alivunjika uti wa mgongo kwa kudaiwa kupigwa na mwalimu, Focus Mbilinyi wa Shule ya Msingi Madeke.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake juzi, Mtaalamu wa Tiba Viungo,Husseni Saidi alisema  alimfahamu Manga wakati huo alipopelekwa mwaka 2017 kupata matibabu, lakini tatizo lake lilikuwa kubwa.

‘’Wakati analetwa tatizo lake lilikua na wiki moja, kulingana na tatizo lenyewe alipewa maelekezo na kurudishwa Hospitali ya Rufaa Kibena kwa ajili ya matibabu zaidi’’alisema Saidi.

Alisema Julai 17, mwaka huu walimpokea tena na kumfanyia uchunguzi  na kubainika amevunjika uti wa mgongo.

‘’Misuli yake imeisha,baadhi ya jointi azina mijongeo mizuri kwa sababu ya misuli kuisha, kuna vitu alishaanza kupata kama vile vidonda kwa sababu hajiwezi kulala muda wote japo, wazazi walifanya juhudi vimeshatibiwa na vyengine vimeanza kupona’’alisema.

Alisema baada ya kumfanyia vipimo, ataanza kufanyiwa tiba rasmi siku.

‘’Baada ya kumfanyia uchunguzi,tumeongea mengi za mzazi, tumeona mambo muhimu ni mawili kitu cha kwanza  mtoto anahitaji kuendelea na huduma ya utengemavu,kupata mazoezi tiba kwa muda mrefu zaidi ili kuzuia asipate yale madhara yatokanayo,’’alisema.

“Kitu cha pili, kumsaidia apate haki zake za msingi, hasa haki ya kupata elimu bada ya kujadiliana na mzazi, tukaamua abaki hapa aanze huduma,tulifanya mpango kuhusu shule tumefanikiwa mawasilianao na shule jumuishi ya jirani ya Ilembula,’’alisema.

Kwa upande wake, baba mzazi  Boniface  Manga alisema tangu wafike hospitali hapo wana siku ya nne wanaendelea kupata tiba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Salum Hamduni aliliambia gazeti hili si muda mrefu kesi hiyo itarudi mahakamanii, baada ya ile iliyofunguliwa mwaka 2017 kufutwa.

Hosea Manga, alifanyiwa tukio hilo Machi 21, 2017 kwa kuadhibia viboko 10,baada ya kukosa hesabu darasani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles