24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito waandaliwa vifaa vya kujifungulia

Na Florence Sanawa, Kilwa

WANAWAKE wajawazito wapatao 150 wananufaika na huduma ya uzazi bora katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ wilayani Kilwa mkoani Lindi, kutokana na kijiji hicho kupata mapato ya uvunaji wa misitu ambayo yanakua kila mwaka hadi kufikia milioni 90 kwenye akaunti ya kijiji hicho.

Akizungumza na MTANZANIA, Mjumbe wa Kamati ya Kijiji ya Misitu, Maimuna Hemed, alisema kutokana na kijiji kukusanya mapato yanayokuwa kutokana na utunzaji na uvunaji wa misitu, kijiji kimejipanga kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kumkinga mama ili aweze kupata uzazi salama.

Alisema kuwa huduma hizo zinatokana na mapato hayo ni zimekuwa na matokeo makubwa kwa jamii hivyo kuipa nafasi jamii yao kunufaika kwa upande wa kuwasaidia wamama wajawazito ili waweze kununulia vifaa vya kujifungulia ili kupungua vifo vya mama na watoto.

Hemed alisema kuwa wanawake wengi walikuwa wakishindwa kugharamia vifaa vya kujifungulia hali ambayo ilikuwa ikichangia wanawake wengi kujifungulia nyumbani hivyo kuhatarisha maisha yao.

Alisema kuwa ili kunusuru maisha ya mama na mtoto, Kamati ya Kijjiji ya Misitu ilikaa na kukubaliana mapato hayo yatolewe kwa wanawake wajawazito wanaokaribia kujifungua.

Hata hivyo, aliongeza kuwa pamoja na changamoto ya kutokuwepo kwa zahanati ya uhakika, lakini wanajitahidi kutumia mapato hayo ili kusaidia huduma ya uzazi ambayo kwa muda mrefu imekuwa na ikihitajika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles