26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wajasiriamali wapata dola 480,000 toka UBA, TEF

Christina Gauluhanga-Dar es salaam



MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya UBA, Isiaka Usman, amesema maono ya Taasisi ya Tony Elumelu (TEF), ni kuondoa vikwazo ambavyo wajasiriamali kutoka Afrika wanapitia wakijitahidi kuinua biashara zao kutoka kuwa ndogo hadi ya kati hadi makampuni makubwa kitaifa na kimataifa.

Ameyasema hayo leo alhamisi Novemba 22, 2018 jijini Dar es Salaam katika hafla iliyowakutanisha wajasiriamali waliopata ufadhili kutoka Taasisi ya Tony Elumelu na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira na Vijana, Antony Mavunde.

Amesema hatua hiyo ni maono ya mwanzilishi wa makampuni ya Heirs Holding kutoka Nigeria, ambapo pia ni mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa United Bank For Africa ( UBA) yenye matawi 20 barani Afrika.

“Katika miaka saba tangu Taasisi kuanzishwa, TEF ilichukua muda kutafakari kasi ya taasisi za ndani na kuanza kubadilisha hadithi kimataifa na kuhamasisha ujasiriamali wa Afrika.

Ameongeza kwa kusema malengo ya baadaye ya Taasisi ya Tony Elumelu, ni kuweka mipango thabiti kuwasaidia wajasiriamali kutoka Afrika kupitia Programu ya Ujasiriamali ya Taasisi ya Tony Elumelu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles