Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Wajasiriamali nchini wametakiwa kufanya biashara zao kisasa ili kuendana na teknolojia huku wakiaswa kuwa waaminifu kwa wateja wao.
Wito huo umetolewa leo Mei 24 jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa mfumo wa kidigatal wa biashara na bidhaa kwa ajili ya wajasiriamali wanawake (Isoko) na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya ambapo amesema kuwa uwepo wa mfumo huo utawasaidia upatikanaji wa masoko kwa urahisi ndani na nje ya nchi.
“Wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kutangaza soko la Afrika, Serikali imeweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara hivyo wanapaswa kuboresha biashara zao na kuwa wazalendo kwa kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi na pato la Taifa,” amesema Wambuya.
Amesema moja ya changamoto kubwa ni ukosefu wa soko la bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali mfumo huo unaenda kutatua changamoto hiyo.
Wambuya amesema pamoja na kuanzisha mfumo huo wanatakiwa kuelimisha watu wanaweza kuona bidhaa ulimwenguni kote zinazalishwa nchini na bora.
“Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara hivyo basi nitoe rai kwenu wajasiriamali kuingia kwenye mfumo huu wa Isoko ili mtangaze bidhaa zenu Kwani mtakuwa mnaitangaza nchi na kuinua uchumi wetu”amesema
Nae Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake (TWCC ), Mercy Sila amesema kuwa ametoa rai Kwa wafanyabiashara kutengeneza bidhaa zinazokubalika sokoni Kwani soko la Tanzania Sasa hivi limekua sana na serikali imeweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara
Aidha, amesema kuwa TWCC inazaidi ya wanawawake 10,000 ambao wanafanya nao kazi hivyo anaamini kupitia mfumo wa iSoko utasaidia kukuza na kuinua vipato vya wanawake hao na kujitangaza na kuitangaza bidhaa zao kimataifa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Afrika nchini, Monica Hangi amesema wajasiliamali wanapaswa kuthubutu hata kam mitaji Yao midogo Kwani hyoi ni fursha Kwao hivyo wanapaswa kuongeza uaminifu na kuboresha bidhaa.
“Hii ni fursa kwenu wajasiliamali kujitangaza lakini hakikishine mnatangaza bidhaa nzuri na zenye viwango zililokidhi vigezo msitangaze bidhaa ghafi hii itasaidia kuitangaza nchi yetu mfumo huu haujamuacha mfanyabiashara hata kama unaotumia simu ya tochi unaweza kujiunga,” amesema Hangi.