25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge na Waziri wa zamani Herman Kirigini afarik dunia

Na Shomari Binda, Musoma

Aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo,Herman Kirigini, amefariki dunia.

Akizungumza na Mtanzania Digital kwa njia ya simu,mtoto wa marehemu na kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Paul Kirigini, amesema Mzee Kirigini amefariki Mei 23, katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara.

Paul amesema amepokea taarifa za kifo cha Mzee Kirigini kwa masikitiko makubwa kwa kuwa bado walikuwa wakihitaji ushauri wake.

“Tunasema haya ni mapenzi ya Mungu yametimizwa hapa duniani, kilichobaki ni kumuombea na kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa baadae,” amesema Paul..

Paul amesema msiba wa mzee Kirigini upo nyumbani kwake Kata ya Kamnyonge Manispaa ya Musoma na taratibu nyingine za mazishi zinaendelea.

Marehemu Herman Kirigini, amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kwa kipindi cha mika mitano kuanzia 1980 hadi 1985 huku akishika wadhfa wa Waziri wa Kilimo na Mifugo.

Pia amewahi kushika nyadhfa mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles