28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waitara kuongoza wanahabari kupanda Mlima Kilimanjaro

Na ASHA MUHAJI-MOSHI

MKUU wa Majeshi Mstaafu, George Waitara, leo atawaongoza waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya Uhuru inayotarajia kaudhimishwa Desemba 9, mwaka huu.

Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), ataongoza msafara wa watu 40 kupanda mlima huo.

Mbali na waandishi wa habari, msafara huo wa siku sita, pia utahusisha washiriki kutoka taasisi za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), maofisa wa Tanapa, washiriki kutoka Taasisi ya Mkapa Foundation na marafiki wa Tanzania waliotoka nchini China.

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya kupanda mlima huo jana, Waitara alisema zoezi hilo linaratibiwa na Tanapa na kwamba mbali na kuhamasisha utalii wa ndani, pia litafanyika kama sehemu ya maadhimisho ya siku hiyo ya uhuru.

“Tumekuwa tukipenda kuhusisha askari wa JWTZ kwa kuwa ndio waliohusika pia kupandisha bendera ya Taifa baada ya tukio la nchi kupata uhuru Desemba 9, mwaka 1961.

“Tunatangaza utalii wa ndani, lakini tunalifanya tukio hili wakati huu tukiadhimisha sikukuu ya uhuru kwani tunakumbuka pia tukio la Luteni Alexander Nyirenda aliyepewa jukumu la kupandisha bendera ya Taifa katika kilele cha Mlima Kilimamjaro.

“Huu ni mwaka wa 10 sasa tangu Tanapa waanzishe utaratibu huu mwaka 2008 ambapo kwa tathimini yao imesaidia kwa kiasi fulani kuhamasisha utalii wa ndani,” alisema Waitara.

Msafara huo utapanda mlima huo kupitia Kampuni ya Utalii ya Zara Adventures chini ya ufadhili wa Tanapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles