Benki ya UBA yazindua huduma mpya ya ‘Magic Banking’

0
1289
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isihaka (wa kwanza kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya 'Magic Banking'.

Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam

Benki ya UBA Tanzania imezindua huduma mpya ya ‘Magic Banking’ itakayomwezesha mteja kufanya miamala kwa njia ya simu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Desemba 5, jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma wa benki hiyo, Asupya Nalingigwa, amesema mbali na huduma  ya Magic Banking kufanya kazi kwenye aina yoyote ya simu lakini pia huduma hiyo ni salama, ya haraka pia mteja hahitaji kuwa  na salio la kufanya miamala.

“Huduma ya Magic Banking inamfanya mteja kufanya miamala ya hadi kufikia Sh milioni moja kwa siku kwa kutumia kadi maalumu ya ‘secure pass’ ambayo inaongeza usalama wa mtumiaji,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania, Usman Isihaka, amesema huduma hiyo itamfanya kila Mtanzania mwenye simu iliyosajiliwa kufungua akaunti papo hapo.

“Mteja anayetumja simu ya mkononi bila ya kujali anatumia mtandao gani wa  simu anaweza kufungua akaunti na sisi kwa kupiga *150*70# bila gharama yoyote,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here