24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waitara awataka Wakurugenzi kusimamia sheria za mazingira

Safina Sarwatt, Moshi

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mwita Waitara, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya kote nchini kusimamia sheria ndogo ndogo za mazingira ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza.

Waitara ameyasema hayo jana Januari 11,2021 Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati alipokuwa akizungumza na maafisa watendaji wa Kata pamoja na wa wakuu wa idara wa halmashauri hiyo mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, kuhakikisha wanazisimamia sheria ndoogo ndogo za mazingira zilizopo kwa mujibu wa sheria ili kuhakisha mazingira yanaedelea kutunzwa.

“Niwapongeze sana Manispaa ya halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kwa kuendelea kuisimamia Sheria hizi za mazingira jambo ambalo limesababisha kuendelea kuwa washindi,” amesema.

Aliongeza; “Niwaombe endeleeni kuisimamia sheria hizi na msisite kuwachukulia hatua pale ambapo watendaji wanafanya vibaya katika kusimamia sheria za utunzaji wa mazingira ,”amesema Naibu Waziri Waitara.

Aidha, katika ziara yake mkoani Kilimanjaro Naibu Waziri huyo pia ametembelea mradi kiwanda cha mbolea aina ya mboji ambayo inatumia mali ghafi ya taka ngumu zinazozalishwa kwenye masoko na majumbani pamoja mradi wa dampo la kisasa.

Naibu Waziri Waitara amesema amefurahishwa na utekelezaji wa mradi wa kiwanda chicho cha mbolea ya mboji inayotokana na taka za mboga mboga na matunda zinazozalishwa kwenye masoko ambao uligharimu zaidi ya Sh milion 800.

“Nimefurahishwa sana na mradi huu wa mbolea ya mboji ambayo mali ghafi yake inatokana na taka zinazozalishwa kwenye masoko yetu na majumbani, hii litasaidia kupunguza tatizo uharibifu wa mazingira pia inaleta tija kwa wananchi kutunza taka kwani taka imeshageuka kuwa mali,” amesema.

Aidha, Naibu Waziri huyo pia ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa Dampo la kisasa ambalo litakuwa likizalisha mbolea ya mboji, ambayo ni rafiki wa mazingira.

Waitara ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi huo na Wataalamu wa mazingira kutoka (NEMC), pamoja na Wataalamu wa mazingira wa Manispaa, mradi ambao ujengwa katika kijiji cha Mtakuja na kuridhishwa na mradi huo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu, amesema kumamilika kwa dampo hilo umekuwa msaada mkubwa wa kuondosha changamoto ya taka ngumu ambazo zinazalishwa kwenye maeneo mbalimbali na kukosa eneo la kuhifadhi.

Aidha, ameongeza kusema kuwa “Manispaa tulikuwa na dampo katika eneo la Karoleni, dampo lile limejaa hali ambayo ilikuwa ikihatarisha usalama wa afya kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka dampo hilo, ” amesema Raibu.

Naye msimazi wa mradi huo, David Kimaro amesema mchakato wa ujenzi wa dampo hilo ulianza tangu mwaka 2019, hadi kukamilika kwake umegharimu kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 2.5 na kwamba ujenzi wa dampo hilo unasimamiwa na kampuni ya ukandarasi ya Rocktrotinic Ltd. ya mjini Moshi.

Awali, akizungumza Afisa afya Mazingira Manispaa ya Moshi Sebastian Mgeta amesema zoezi la ukusanyaji taka linatekekezwa na halmashauri hiyo kwa asilimia 100.

“Taka zinazozalishwa na Manispaa ya Moshi ni tani 286 kwa siku , ambapo halmashauri tani 185 kwa siku na tani 15 zinazozalishwa huwa zinatumika kwa uzalishaji kwa njia ya marejei kwa ajili ya matumizi mengine,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles