Na  Sheila Katikula, Mwanza
WAUMINI wa dini ya Kiislamu na Madhehebu mbalimbali nchini wameombwa kujiwekea utaratibu wa kutembelea vituo vya watoto yatima ili waweze kuwashika mkono kwa kutoa sadaka kwenye vituo vya kulelea  watoto hao kama sehemu ya kurejesha.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa Msikiti wa IBADH uliopo jijini Mwanza, Nouh Mousa alipotembelea kituo kinachotoa malezi na makuzi kwa watoto yatima cha SOS Children’s Village kilichopo jijini Mwanza.
Mousa alisema ni vema wananchi kuweka utaratibu wa kutoa sadaka kwa watoto hao ambao wamepoteza wazazi wao ili kuweza kuwapa faraja na kuwarejeshea matumaini yaliyopotea.Â
Amesema katika adhimiaho la Eid, waamini wa msikiti wa Ibadh kwa kushirikiana na jumuiya ya Istiqama wal kwenye Kituo hicho ya vitu mbalimbali  vyenye thamani ya sh milioni 2 na pesa  tasilimu sh 10,0000 kama sehemu ya sadaka ya Eid El Hajj.
“Hakuna ibaada nzuri kama ya kuchinja, Mtume s.a. w anasema mwanadamu mbali na kufanya mema, lakini kwenye sikukuu ya Eid kuchinja kuna leta baraka katika maisha yetu na furaha katika familia zetu na majirani.
“Tunaendelea pia kuhimiza kujenga vituo vya kulelea watoto yatima  kila sehemu kwa sababu Mwenyezi Mungu kuwaondoa wazazi wao wakiwa bado watoto wadogo  jukumu la kuwalea tumeachiwa sisi, sasa tukipuuza kiwajali na kuwathamini tutaulizwa siku ya kiama na hata kukosa baraka maishani,” amesema Mousa.
Naye mwakilishi wa kampuni ya mafuta ya GBP mkoani hapa, Sood Ally amesema lengo la kutembelea kituo hicho ni kuwatia moyo walezi ambao wanalea watoto hao ili waweze kutambua kuwa jamii inawathamini na kuwajali na inatambua umuhimu wao.
Naye Mratibu Malezi Mbadala wa kituo hicho, Anthony Mkinga alisema kituo hicho kina watoto 88 wakiwemo wakike 38 na wakiume 50  ameiomba jamii  kusaidia masuala ya elimu, afya na mavazi kwa watoto hao.
“Sisi tunafanya kazi na Serikali na watoto wao tunawapokea kutoka kwenye ofisi ya Ustawi wa jamii wanawafatilia kwa kina wapojilidhrisha wana sifa za kuwaleta kwenye kituo chetu wanawaleta na sisi tunawapokea,” alisema Mkinga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Sos, Tanzania Bara na Zanzibar, David Mulongo aliwashukuru wadau hao kwa kuona umuhimu wa kutembelea watoto hao kwani zaidi ya asilimia 60  ya watoto waliopo kwenye vituo si kwa kupenda bali ni kwa sababu ya changamoto za kimaisha.