22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Walengwa Tohara Kinga Simiyu wasuasua

Na Derick Milton, Simiyu

Mpango wa Tohara Kinga kwa Wanaume na Vijana katika Mkoa wa Simiyu, ambao unalenga kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa vijana umeendelea kukumbwa na changamoto ya mwitikio hafifu wa kundi hilo lengwa.

Katika mpango huo ambao unatekelezwa katika Halmashuari zote sita za mkoa huo, kuanzia Oktoba 2020 hadi Juni, 2021 umewafikia wanaume wakiwemo watoto 58,516 kati ya walengwa 83,000 wanaotarajiwakufikiwa kufikia Oktoba mwaka huu.

Hayo yameelezwa jana Jumanne Julai 20, 2021 na Mratibu wa Ukimwi mkoa, Dk. Hamis Kulemba wakati wa kikao cha wadau wa afya ambacho kililenga kuonyesha utekelezwaji wa mpango wa Tohara kinga mkoani humo.

Dk. Kulemba amesema lengo mpango huo wa tohara nikupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, ambapo vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 24 ndiyo walengwa zaidi.

“Licha ya mpango kufanikiwa kwa kiwango kikubwa mpaka sasa, lakini wengi ambao wamefanyiwa tohara ni watoto wadogo, wale ambao tunawalenga zaidi kwa maana ya vijana wa miaka 20 hadi 24 ni wachache sana kujitokeza,” amesema Dk. Kulemba.

Amesema vijana wengi wenye umri huo wamekuwa wagumu kujitokeza kufanyiwa huduma hiyo licha ya kuwepo wengi ambao hawajafanyiwa tohara, huku akitaja sababu kubwa kuwa ni aibu, mila na desturi pamoja na kutojali.

Amesema kuwa wameendelea kuhamasisha jamii hasa vijana hao kwa ajili ya kujitokeza kwa wingi kufanyiwa tohara, ambapo mpango huo unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na shirika la IntraHealth.

Aidha, Dk. Kulemba ameeleza kuwa wameanzisha mpango mkakati wa kufanyia tohara watoto wadogo, ambapo umeanzia katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu na utatekeleza katika hospitali zote za wilaya.

Kwa upande wake, Ofisa Mpango kutoka Wizara ya Afya, Baraka Mpora, amesema kuwa mikoa yote ambayo mpango huo unatekelezwa mafanikio yameanza kuonekana kwa kupunguza kiwango cha maambukizi mpya ya VVU.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles