28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waislam waipongeza Serikali kukubali maoni yao kuhusu somo la dini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAISLAM nchini wamempongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda kwa kukubali kusikiliza maoni yao juu ya mtaala wa masomo ya kiislam .

Akizungumza Agosti 16, 2023 Amiri wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Mussa Kundecha ameeleza kuwa Viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na Islamic Panel wamekutana na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda na kuhitimisha mazungumzo yao kwa kukubaliana.

Awali, viongozi hao wa dini walikuwa wanalalamika juu ya mtaala mpya wa elimu ya dini ambao ulitarajiwa kufundishwa kwenye shule za msingi na Sekondari nchini kuwa haukuwa na misingi ya kiimani ya dini hiyo.

“Tunamshukuru Waziri wa Elimu alitusikia ombi letu na aliomba tukutane nae kwa ajili ya mazungumzo,” mesema Kundecha.

Alisema kuwa Siku ya Agosti 12, Waziri na wataalam wa Wizara hiyo walikutana na viongozi hao kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao.

“Tulikutana na Waziri siku ya Jumamosi akiwa na wataalamu wake wa taasisi ya elimu tulizungumza na kukubaliana,” amesema.

Amesema kuwa makubaliano yalikuwa ni kwamba umiliki wa mitaala ya somo la dini utabaki kwa wenye dini wenyewe kama ilivyokuwa zamani.

“Suala la dini na imani haviwezi kutenganishwa kwani imani ndio msingi wa mafundisho ya dini,” alihitimisha Kundecha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles