27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wahudumu wa Afya Usangi wanaoipaka matope serikali waonywa

Safina Sarwatt, Mwanga

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Salehe Mkwizu amekemea tabia za baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali ya wilaya ya Usangi, kuwatoza wajawazito fedha huduma za kujifungua jambo ambalo ni kinyume na taratibu za wizara ya afya.

Mkwizu ameyasema hayo Jana Desemba 10, kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Halmashauri hiyo, baada ya hafla fupi ya kuapishwa kwa madiwani hao, pamoja na uchaguzi wa mwenyekiti wa baraza na makamu mwenyekiti ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Jumuiya ya Wazazi Mwanga.

Amesema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi kuhusu hospitali ya wilaya kuwatoza fedha za huduma za kujifungua kwa viwango tofauti ambapo kwa huduma za kujifungua kwa njia upasuaji ni 130,000 hadi 150,000, bila kutoa risiti.

“Jambo hili limenisikitisha sana imenifedhehesha pia kwa sababu huduma za kujifungua kwa wajawazito wizara ya afya imeelekeza ni bure lakini leo hii wanatozwa fedha, tatizo hilo linaipaka serikali matope,” amesema Mkwizu.

Mkwizu pia amewataka madiwani kwenda kutoa elimu kuhusu huduma za afya kwa wajawazito ili kukomesha tabia hizo katika hospitali za serikali.

Aidha, katika uchaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye ni diwani wa kata Shighatini, Salehe Mkwizu ameibuka msindi kwa kupata kura 28, huku Makamu Mwenyekiti, Mohamed Abdallah akipata kura 28 sawa na asilimia 100 za kura zilizopigwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles