Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya TMS Consultants LTD inatarajia kuzindua programu mpya ambayo itasaidia kuondoa tatizo la ajira kwa vijana hasa wale wanaosoma vyuo vikuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Sebastian Kingu alitoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na vyuo vingine vya elimu ya juu kuhudhuria uzinduzi huo.
“Program hii inahusu ‘Digital online memtorship internship training for employment creation progranne’ uzinduzi wake utafanyika siku ya Oktoba 3 mwaka huu tunaangazia kupunguza tatizo la ajira zilizo rasmi kwa vijana wa Tanzania.
“Hapa nchini takribabi asilimia 68 ya idadi yote ya watu ni ya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kulingana na sense ya 2012 na watu hawa wako katika kundi la vijana,vilevile takribani vijana 800,000 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka.
“Hii inamaanisha kuwa vijana wote wanaomaliza masomo kuanzia shule za msingi ,sekondari na vyuo mbalimbali ni vijana asilimia tano tu ndio wanabahatika kupata ajira katika sekta rasmi za umma na binafsi waliobaki asilimia 95 hawana ajira ambayo sio rasmi,” alieleza Kingu.
Alisema ukosefu wa ajira huweza kufanya vijana wengi kujiingiza katika vitendo viovu kama vile matumizi ya dawa za kulevya,ulevi kupindukia, ukahaba na mengineyo.
“Lakini hali hii ikiachwa na kuendelea kukua inaweza kufika kiwango kibaya zaidi kwa vijana kuweza kurubuniwa na watu ambao hawaitakii mema nchi na hata wengine wanaweza kurubuniwa kwa kujiingiza kwenye makundi ya kigaidi hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuleta machafuko,” alisema.
Alisema walengwa hasa kwa kipindi cha mwanzo ni vijana wanasoma vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu wanasoma masomo ya shahada ya kwanza ambao watapata ajira iliyorasmi angali bado wakiwa wanafunzi kabla ya kumaliza masomo ya chuo.
“Maelezo zaidi ya napatikana katika tovuti ya www.tmsconsultants.co.tz hivyo tunawakaribisha wote uzinduzi utafanyika siku ya Jumamosi hoteli ya Peacock jijini hapa .
“Na mradi huu utatekelezwa kwa kushirikiana na washiriki wa kimkakati anbao ni Enterprise Finance(EFL),Madson Property Co.ltd,Salvation Farm and Markerting Co.Ltd, Agricom Africa Ltd,Elshorouk Co ltd,Surveying Equipment Center(EA) Ltd na zingine nyingi washiriki watakuwepo siku ya uzinduzi,”alisema.