25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Ugonjwa kichaa cha mbwa usihusishwe na ushirikiana

Na  AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kuacha kuhusisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa na imani za kishirikina, badala yake mtu anapong’atwa na mnyama huyo awahi hospitali kupata matibabu.

Akizungumza na MTANZANIA, Dar es Salaam wakati wa mahojiano, mtaalamu wa afya ya jamii kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,  Jubilate Bernard alisema  wapo watu katika jamii wanahusisha dalili za ugonjwa huo na mambo ya kishirikina kitu ambacho sio sahihi.

“Siku ya kichaa cha mbwa  huadhimishwa kila Septemba 28, duniani ambapo jumuiya ya kitaifa inatoa elimu juu ya ugonjwa huo  kwa duniani nchi ya India inaongoza kuwa na ugonjwa na  kufuata bara la Afrika.

“Watu  5,9000  hupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa  asilimi 96 ni Afrika na asilia  huku asilimia 36 ni Afrika, kwa Tanzania kunatakwimu za wanaokwenda hospitali mwaka  jana  watu walioripoti kung’atwa na mbwa ni  12,680  nchi nzima ,kati yao ni watu sita walifariki.

“Mwaka huu, wamepatikana na watu 18,766 mfumo haujaripoti vifo,wengine  wanahusisha na ushirikina kutokana na dalili zake kwahiyo wengine wanaenda kwa waganga wa kienyeji na wanafariki,”alieleza.

Alisema utafiti uliofanyika mwaka 2002 makadirio ya baadhi ya maeneo  yalionesha  kuwa vifo  vinavyotokea ni  1500.

“Waathirika wengi ni watoto wa chini ya miaka 15 wengine hawaripoti mpaka baadae dalili zinapoanza kuonekana  ninachowaambia jamii kwanza huo ugonjwa ili kuushinda wawachaje mbwa na paka kila mwaka (chanjo ya kichaa cha mbwa).

“Wawafungie wanyama ndani wawafungulie usiku,pia kunawa watu wanazoea mbwa wa ndani hadi mbwa anamlamba mtu hata kidonda hivyo virusi vinaweza kuingia  na jeraha ikikutana na mate ya mbwa unaweza kupata madhara,”alisema.

Alisema mtu aking’twa, anatakiwa kusafisha jeraha kwa maji tiririka  na sabuni kwa dakika kumi au zaidi na jeraha hilo haliruhusiwi kufungwa badala yake muhusika awahishe kituo cha afya na kupata chanjo zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles