27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wahitimu vyuo kupatiwa stadi za ajira

Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya TMS Consultants LTD inatarajia kuzindua programu mpya ambayo itasaidia kuondoa tatizo la ajira kwa  vijana hasa wale wanaosoma vyuo vikuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Sebastian Kingu alitoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu  pamoja na vyuo vingine vya elimu ya juu kuhudhuria uzinduzi huo.

“Program hii inahusu ‘Digital online memtorship  internship training for employment creation progranne’ uzinduzi wake utafanyika siku ya Oktoba 3 mwaka huu  tunaangazia  kupunguza tatizo la ajira  zilizo rasmi kwa vijana wa Tanzania.

“Hapa nchini takribabi asilimia 68 ya idadi yote ya watu  ni ya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kulingana na sense ya 2012  na watu hawa wako katika kundi la vijana,vilevile takribani vijana 800,000  huingia kwenye soko la ajira kila mwaka.

“Hii inamaanisha kuwa vijana wote wanaomaliza  masomo kuanzia shule za msingi ,sekondari na vyuo mbalimbali  ni vijana asilimia tano tu  ndio wanabahatika kupata ajira  katika sekta rasmi za umma na binafsi waliobaki asilimia 95 hawana ajira ambayo sio rasmi,” alieleza Kingu.

Alisema ukosefu wa ajira huweza kufanya vijana wengi kujiingiza katika  vitendo viovu  kama vile matumizi ya dawa za kulevya,ulevi kupindukia, ukahaba na mengineyo.

“Lakini hali hii ikiachwa na kuendelea kukua  inaweza kufika kiwango kibaya zaidi kwa vijana  kuweza kurubuniwa  na watu ambao hawaitakii mema nchi  na hata wengine wanaweza kurubuniwa kwa kujiingiza kwenye makundi ya kigaidi hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani  na kuleta machafuko,” alisema.

 Alisema walengwa hasa kwa kipindi cha mwanzo ni vijana wanasoma vyuo vikuu  na vyuo vingine vya elimu ya juu  wanasoma masomo ya shahada ya kwanza ambao watapata  ajira iliyorasmi  angali bado wakiwa wanafunzi  kabla ya kumaliza masomo ya chuo.

“Maelezo zaidi ya napatikana katika tovuti  ya www.tmsconsultants.co.tz hivyo  tunawakaribisha wote  uzinduzi utafanyika  siku ya Jumamosi  hoteli ya Peacock jijini hapa .

“Na mradi huu utatekelezwa  kwa kushirikiana na washiriki wa kimkakati  anbao ni Enterprise Finance(EFL),Madson Property Co.ltd,Salvation Farm and Markerting Co.Ltd, Agricom Africa Ltd,Elshorouk Co ltd,Surveying Equipment Center(EA) Ltd na zingine nyingi washiriki watakuwepo siku ya uzinduzi,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles