25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wa saratani waongezeka kwa kasi

Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

Mkurugenzi  wa huduma za Kinga ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa amesema idadi ya wagonjwa wa saratani imeongezeka kutoka 250  na  300 kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita hadi kufikia  wagonjwa 900.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam kuelekea mwezi Oktoba wa saratani ya matiti alisema hii ni ongezeko la mara tatu ya kipindi cha miaka mitatu  iliyopita.

“Takwimu za saratani nchini  zilizotolewa na shirika la Global Khan ambao ni  wadau wakubwa wa shirika la afya Duniani, inaonesha kuwa kipindi cha mwaka 2018 /2019 wagonjwa wapya 42,000 hugundulika na saratani  nchini.

“Lakini ukiangalia takwimu  za hospitali  asilimia 29 wamefika hospitali ni kwamba watu 12,625 pekee waliweza kuonwa katika vituo vya afya na  kati ya hizo saratani ya matiti imechukua asilimia 13.

“Tukiangalia takwimu za saratani ya matiti kwa Ocean Road  kwa mwaka 2018/2019 tuliona wagonjwa 963 ambao walichukua takribani asilimia 16 ya wagonjwa wote na saratani ya matiti ilichukua nafasi ya pili kwa wanawake na ya tatu kwa zote.

“Tukilinganisha takwimu zetu za miaka 10 iliyopita na sasa kunatofauti ya idadi lakini pia umri unaoathirika tukiangalia idadi ya wagonjwa kati ya 250 na  300 kwa kipindi hiki tumeona hadi wagonjwa 900,” alieleza Dk Kahesa.

Alisema kuwa wastani wa  umri wa waathirika kwa miaka 10 iliyopita  ni miaka 64 lakini  kwa sasa ni miaka  56.

“Hii maana yake ni miaka saba  chini ya umri  wa kipindi cha nyuma kwahiyo ugonjwa wa saratani ya matiti umekuwa ukiongezea na pili  umri wa waathiri nao umeshuka chini.

SABABU YA UGONJWA KUONGEZEKA

Dk Kahesa alisema sababu kubwa ya ugonjwa kuongezeka ni mabadiliko ya mfumo wamaisha katika kipindi cha miaka 10.

Alitaja mabadiliko hayo kama ulaji mbaya ambao unaweza kusababisha uzito mkubwa kwa watu huku wakiwa hawaelewi hatari yake.

“Nikisema mfumo bora wa maisha namaanisha ulaji wa vyakula ambao si sahihi mfano mtu anakula bila kuzinagati kanuni zinazotakiwa yam lo kamili badala yake uzito unaongezeka na kusababisha matatizo mbalimbali kama saratani na mengine.

“Kitu kingine ni kutokufanya mazoezi sasa utakuta mtu anakula kupita kiasi halafu hafanyi mazoezi sehemu ya kutembea anatafuta usafiri sikuhizi hata kupanda ngazi watu hawataki wanataka tu lifti sasa mfumo huu ni mbaya,” alibainisha Dk Kahesa.

Alisema sababu zingine ni matumizi ya vile kama vile tumbaku na  pombe.

“Hivi navyo vinasababisha kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani watu wengi wanatumia ila hawajui madhara yake ya baadae,” alisema.

ELIMU KUTOLEWA KWA NJIA YA MTANDAO

Dk Kahesa alisema kutokana na hilo taasisi imeamua kuchukua fursa ya mwezi  wa 10 ili  kuweka jitihada mahususi ya kupambana na ugonjwa huo.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa jamii lakini pili itabidi  tupanue wigo wa kutoa elimu kwa jamii  kwa makundi ya wanafunzi wa vyuoni na sekondari Lakini  pia jamii hasa wale ambao wako pembezoni tumeona changamoto ya kuwafikia  na suala la elimu bado liko chini na taasisi imeamua kuwa na kitengo mahususi  kwaajili ya kutoa taarifa na elimu kwa jamii ukizingatia saratani zote .

“Tutatoa fursa kwa jamii kuwasaliana na sisi moja kwa moja kutoka sehemu mbalimbali kwa njia ya mawasiliano ikiwemo simu na pili mitandao ya kijamii ikiwemo isntagram na whats ap na nyinginezo,” alisema Dk Kahesa.

Pia alifafanua kuwa wanatarajia kuboresha mfumo wa rufaa wa wagonjwa na pia inakaribisha kufanya uchunguzi wa awali wa watu wenye changamoto.

“Tukija kwa upande wa vitendanishi na vifaa serikali imenunua mashine ya kisasa ambayo imetengenezwa  mwaka 2019 na  imenunuliwa kwa Sh milioni 189 na   imesimikwa hapa na itaanza kutumika rasmi  mwezi huu wa 10.

“Tunatarajia mashine hii itasaidia jamii kwani itapima  zaidi ya watu 35,000  kwa mwaka na inaweza kugundua zaidi ya kinamama 100 wenye saratani ambao walikuwa hawapati huduma hii nchini  na kwa kutumia mashine hii itagundua mapema na itapunguza idadi ya kubwa ya watu wenye vivimbe vya awali ambao wanasaratani kwenye hatua za mwanzo,”alibainisha Dk Kahesa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles