20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Damu Salama kukusanya chupa 32,700

MPANGO wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) umesema unatarajia kukusanya chupa za damu 32,700  nchi nzima ili kuokoa maisha ya akinamama wanaojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Akizungumza na MTANZANIA katika Mahojiano maalum, Mkuu  wa Idara ya Ukusanyaji damu, Dk Aveline Ngasa alisema ukusanyaji damu huo unaambatana na kampeni iliyoanza jana Septemba 21 hadi 25 kwa kulenga maeneo yote ya mijini na vijijini.

Alisema katika kampeni hizo za ukusanyaji damu kauli mbiu ni ‘Damu salama Uhai wa Mama’

“Ukosefu wa damu unasababisha vifo vya kinamama ambapo  moja ya tatu ya vifo hutokea kwasababu hiyo  na ripoti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  ya mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kuna vifo 556 kwa kila kizazi 100,000 na vifo hivyo ni asilimia 18  ya vifo vyote vya wanawake wenye umri chini ya miaka 15-49.

“Mama napoenda kujifungua katika kituo cha afya anaweza kupata shida ya kuvuja damu na akahitaji kuongezewa lakini kama  haipo ataongezwa nini? Hii husababisha kupoteza maisha,” alisema Dk Aveline.

Alisema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujitokeza kuchangia damu na kufikia lengo la ukusanyaji damu katika kampeni hizo.

“Hadi sasa kiasi cha mwitikio sio kidogo watu wanajitokeza kuchangia damu lakini tunataka kufikia matarajio yetu hivyo tutaendelea kuhamasisha watu wajitokezwa zaidi.

“Kila mwaka uhitaji wa damu ni chupa 550,000   hii ni sawa na asilimia  moja ya idadi ya watanzania  na tumejigawa kwa timu ya Halmashauri 185  wanatakiwa kukusanya chupa 150 kwa kila mmoja,hospitali za kanda  chupa 500,timu ya mikoa  chupa 150  na timu ya damu salama  vituo vya kanda chupa 500,” alisema Dk Aveline. 

Alisema  Kanda ya kusini imehamasika zaidi katika zoezi la uchangiaji damu hivyo yapo maeneo ya vijijini yanahamasa kubwa.

Dk Aveline alitoa wito kwa jamii kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kufanikisha kampeni hizo.

“Jamii  hasa vijana  wajitokezea kuachangia damu kuanzia umri wa miaka 18 hadi 65 ndio wanaruhusiwa kutoa damu, uzito unaotakiwa ni kuanzia kilo 50 na mchangiaji asiwe na ugonjwa wowote,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles