24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wagombea Chadema wanyukana majimboni

 MWANDISHI WETU– NJOMBE

JOTO la uchaguzi limezidi kupanda katika Jimbo la Njombe Mjini, ambapo wagombea tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Njombe kujitokeza na kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera za chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza jana mjini hapa, Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga ni mmoja ya wagombea waliojitokeza kuwania tena jimbo hilo kwa kuchukua na kurejesha fomu.

Alisema pamoja na yaliyotokea kuanzia mwaka 2015, uongozi umeshindwa kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo la Njombe Mjini.

“Pamoja na yale yaliyotokea yote, kipindi cha miaka mitano tumeona bado uongozi umeshindwa kutatua changamoto ambazo sisi ilikuwa ni ajenda zetu 2015, asilimia 80 ya wananchi wa Jimbo la Njombe Mjini ni wakulima hatujawahi kupata mbunge ambaye amejipambanua kuwatetea wakulima bungeni.sasa kwa mara nyingine tena nimekuja kuomba ridhaa ya chama changu,” alisema Masonga

Mbali naye pia yupo Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba ambaye naye alichukua fou na kurudisha kuomba kuteuliwa kuwania ubunge katika jimbo hilo.

Alisema kuwa kilichomsukuma kugombea ni maono yake ya kupata kiongozi mwingine mwenye maono mapya.

“Njombe ina viongozi wapya waliotangulia lakini mimi nimeona iko sababu ya kupata kiongozi mwingine mwenye mtazamo mpya, mawazo mapya na fikra mpya ili tuweze kuitengeneza Njombe iliyo mpya, hatuwezi kuitengeneza Njombe mpya.

“… kwa mawazo ya ya zamani kwa hiyo ninaamini ninayo mawazo mapya mazuri ambayo yanaweza kuibadilisha Njombe yetu na ikawa moja kati ya maeneo bora Tanzania,” alisema Rose Mayemba

Mgombea mwingine aliyerejesha fomu ni Mariet Joseph Mwalongo ambaye alisema vipaumbele vyake ni ofya, elimu na maji na kuahidi endapo akipata nafasi ni lazima aweze kuvipigania

“Afya, Kilimo. Natamani kuona mabadiliko kwa kusaidiana na wananchi wenzangu, Njombe kila sehemu inatambulika kwa kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, nasimama kama kijana, mama kutafuta suluhisho,” alisema Mariet Mwalongo 

Naye Siglada Mligo, aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Njombe Mjini amerejesha fomu huku akiahidi kwenda kutatau changamoto za wananchi kwa kupambana na kukamilisha miradi ambayo haijaweza kukamilika kwa miaka mingi.

“Mimi ni muumini wa matatizo ya wananchi namna gani tunaenda kutatua matatizo ya wananchi,tuna miradi mingi Njombe ya toka mwaka 2008 lakini Njombe ndio halmashauri pekee Tanzania inayoongoza kwa mapato kwanini miradi haiishi.hayo ndio mambo ambayo natamani nikipata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo la Njombe mjini niweze kupambana na kuyapatia ufumbuzi,” alisema Siglada Mligo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles