27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waganga Wakuu watakiwa kutoa huduma bora za afya

Na Neema Paul, (TUDARCo), Mtanzania Digital

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Afya nchini (National Health Workforce Volunteerism Guideline) imekamilisha mwongozo wa kitaifa wa kuwawezesha wahitimu wa kada za afya ambao hawana ajira rasmi ili waweze kuajiriwa kwa muda na kutoa huduma kwenye vituo vya afya vilivyopo nchini.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba 16, jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri ambapo ajenda kuu ilikuaw ni kujadili namna ya utoaji huduma bora baada ya uwekezaji wa miundombinu uliofanywa na serikali ili kuboresha huduma za afya nchini

Waziri huyo ametoa maelekezo kwa vituo vya afya vilivyokamilika kuanza kutoa huduma za afya za awali mara moja kwa kuwatumia wahitimu wa afya ambao wamehitimu kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea ‘huduma za afya huanza hatua kwa hatua na kwamba hata Muhimbili haijakamilika kutoa huduma zake kwa ubora uliokamilika na unaohitajika.

Aidha, Dk. Gwajima amedai kuwa muongozo huo unatoa utaratibu wa namna bora ya hospitali na vituo vya afya kuweza kutumiwa wahitimu wa kada ya afya ambao hawajaajiriwa ili waweze kutumika rasmi katika utoaji wa huduma za afya kwa njia ya kujitolea

Ameongeza kuwa Serikali kupitia wizara ya afya imefanya uwekezaji mkubwa hivyo ametoa  wito kwa Wganga wote kutoa huduma bora kwa kuzingatia weledi na misingi ya kimaadili ya utoaji huduma bora kwa wananchi ili kuweka uwiano mzuri wa ajira, miundombinu na vifaa tiba ikwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wateja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles