27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wafugaji wawaingiza matatani watumishi wa maliasili

Na MURUGWA THOMAS, TABORA

SERIKALI imesema itawasaka watendaji na watumishi wa Idara ya Maliasili mkoani Tabora, ambao waliwatoza wafugaji tozo zisizohalali na kuwapa stakabadhi zilizoandikwa kwa mkono na fedha hizo zirudishwe kwa wahusika.

Wafugaji na waliopewa stakabadhi zilizoandikwa kwa mkono wametakiwa kuzipeleka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili wahusika wachukuliwe hatua.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Philemon Sengati, wakati wa kikao kazi cha kusikiliza kero za wafugaji kutoka halmashauri zote za mkoa huo.

Dk Sengati alisema Serikali haiwezi kuendelea kukubali kuona wafugaji wanatozwa tozo zinazowaumiza, huku  zikitolewa kwa njia ya vitisho tena kwa kificho katika maeneo ya porini ambako hakuna mtandao wala benki.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema tozo hizo ni zile zinazodaiwa kuwa za meza ambazo hutozwa na watendaji wa vijiji, kata na watumishi wa idara ya maliasili ambazo amesema ni  rushwa hivyo ni lazima ikomeshwe.

Dk. Sengati aliwaomba wafugaji wote ambao wameumizwa na tozo zisizo rasmi, washirikiane na ofisi yake kwa kutoa taarifa ambazo zitafanikisha kuwatafuta  na kuwakamata wahusika wote ili waweze kurejesha fedha za walizochukua.

 â€œTumefanikiwa kurejesha fedha za wakulima wa tumbaku ambao walikuwa wamedhulumiwa na viongozi wasio waaminifu, hatuwezi kushindwa kwa wafugaji’ alisema Dk Sengati.

Katika kikao hicho, pia aliagiza misako yote dhidi ya mifugo ambayo imekuwa ikifanywa na watumishi wa idara ya maliaasili ipate kibali kutoka kwenye ofisi yake ili kuzuia unyanayasi wanaofanyiwa wafugaji.

Mwita Sumaku ambaye ni Mfugaji wa Kipili Sikonge, alisema ng’ombe wake 169 walikamatwa akatozwa Sh milioni tano, lakini stakabadhi aliyoandikiwa ilionyesha  Sh milioni mbili.

Mwita alidai alipojaribu kuhoji uhalali kwa wahusika, aliambiwa akiendelea atapata matatizo zaidi.

Naye mfugaji mwingine toka wilayani humo aliyejitambulisha kwa jina la Moga Maganga alisema ng’ombe wake 84 walikamatwa na kutozwa Sh milioni 6.6 lakini alipewa stakabadhi ya mkono na sio ya kielektoniki kama Serikali inavyoagiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles