26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MOI yaweka historia kwenye upasuaji

Na AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

WATOTO 15 wenye matatizo ya mgongo wazi na kichwa kikubwa, wamefanyiwa  upasuaji wa kisasa  kwenye   kambi maalum ya upasuaji katika Taaisisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa upasuaji huo juzi, Daktari Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Laurent Lemery, alisema hadi sasa wamefanya upasuaji zaidi ya mara 7,000 tangu walipoanza upasuaji huo miaka miatano iliyopita.

Dk Lemery alisema kwasasa wanafanya upasuaji wa kisasa zaidi tofauti na ule wa zamani.

“Katika hiki ni chumba cha upasuaji ambacho kimetengwa maalum kwaajili ya watoto, kuna aina mbili za upasuaji, ya kwanza katika upasuaji wa kichwa kikubwa tunaingia ndani ya ubongo na tunaangalia, aina ya pili ni kuweka mirija kwenye vyumba  vya ndani ya ubongo ambao ndio mara nyingi vinajaa maji hivyo tunatoa maji hayo.

“ Hii operation  ya kwanza  ni mpya  katika ulimwengu wa matibabu na sio sehemu zote inafanyika, pia  tukizungumzia namba kwa ufanyaji wa operasheni sisi hapa MOI  ni wa pili, kuna kituo kimoja tu duniani nakifahamu.

“Sisi pia tunafundisha kuhusu aina hii ya kisasa ya upasuaji kwa Watanzania wenzetu na kwa nchi za jirani hata nchi za Ulaya kama Italia na Uingereza wamejifunza hizo operesheni hapa kwetu,”alisema Dk Lemery.

Alisema kuwa kwa wastani wameweza kufanya operation zaidi ya 7,000 ndani  ya miaka mitano.

Kwa upande wake mfadhili wa upasuaji huo, a mfanyabiashara, Azim Dweji, alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kusaidia watu wasiokuwa na uwezo wa kulipia matibabu kama sehemu ya ibada zao.

“Nimefurahi kuona madaktari bingwa hawa wote ni vijana, inatia moyo kuona vijana wetu wanajituma na hii kazi ya udaktari ni kujitolea kusaidia binadamu.

“Pia nafurahi kusikia kuwa idadi ya kushindwa ni ndogo, niwasihi Watanzania wenzangu kwamba hizo operesheni zinafanyika bure lakini tusaidie serikali kuchangia gharama za matibabu kama 300,000 kila mmoja, wapo wanaotumia  pombe chupa 20 anaweza kuamua kuacha na kutoa kwaaji ya matibabu  ya mtoto mmoja.

“Mwingine anaweza kuuza hata ng’ombe mmoja akawasaidia wenzake, hilo ndilo Mungu anapenda ni wasihi Watanzania kusaidia wengine,”alisema Dweji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles