28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAFUGAJI WATANO WAJERUHIWA

qqqqqqqqqqqqqqqq

Na MURUGWA THOMAS-TABORA

WATU watano wakazi wa Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora ambao ni wafugaji, wamejeruhiwa kwa risasi na mmoja amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete.

Wafugaji hao wanadaiwa kuvamia kambi ya hifadhi ya wanyamapori iliyopo Kijiji cha Utimule Kata ya Ngoywa na kutaka kuchukua mifugo yao iliyokamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu tukio hilo, Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori kutoka Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi, Nasser Alli, alisema wafugaji zaidi ya 40 walijikusanya   na kuvamia kambi kwa lengo la kuchukua mifugo yao.

Alisema usiku mmoja kabla ya tukio,  alipokea simu ya mtumishi mwenzake akimjulisha amepigiwa simu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila, kuwa kuna wafugaji wanataka kuvamia kambi hiyo ili kuchukua ng’ombe wao 200.

Alisema wafugaji waliweza kuvamia kambi hiyo na kuanza kuwashambulia kwa silaha za jadi kama sime, mikuki, upinde na fimbo lakini askari walipambana na  kufanikiwa kuwakamata wafugaji watano huku wengine wakitoroka.

“Kutokana na mapambano hayo ndipo askari wa maliasili walipofanikiwa kuwazidi nguvu na kuwakamata wafugaji watano, kati yao mmoja aliyejulikana kwa jina la Kisena Kubija, alikuwa na majeraha.

“Tuliwapeleka hospitalini kutibiwa kutokana na majeraha waliyokuwa nayo madogo madogo, wanne waliruhusiwa ispokuwa Kubija ambaye bado amelazwa, Yegela Mahondola, Bupolo Lutaja, Shigela Keema, Lugwisha Maduhu, tayari wamefikishwa mahakamani.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Kitete, Dk. Benedicto Komba, alisema alipokea majeruhi hao huku mmoja akiwa amevunjika miguu miwili kwa kupigwa risasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles