23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WALILIA ENEO LA MAKABURI

dscf2789

Na CLARA MATIMO – MWANZA


 

WAKAZI wa kata za Lwanhima na Kanindo zilizopo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa kushindwa kuwatatulia changamoto ya maji, eneo la maziko na umeme ambazo zimekuwa zikiwakabili muda mrefu.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti kuhusu changamoto hizo, wakazi hao walisema ingawa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mery Tesha, alizungumza nao mwaka jana na kuahidi kuwatatulia kero hizo, lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali.

Tatu Kanundo, mkazi wa Mtaa wa Kagera Kata ya Lwanhima, alisema wanatumia maji ya visima ambayo ni machafu lakini hata hivyo inawalazimu kuamka saa 10 usiku ili kuwahi foleni.

“Tunawashangaa viongozi wetu hasa Mbunge, Stanslaus Mabula, ametusahau kabisa wakati aliahidi kututatulia kero hii  alipokuja kutuomba kura mwaka juzi, hajui kama kura hizo tulimkopesha lakini ameenda jumla je, miaka mitano ikiisha atarudi tena kuja kutuomba kura,” alihoji Tatu.

Elizabeth Fumbuka, alimwomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kufika katika kata yao ili ajionee maji wanayotumia kwa kuwa yanatumiwa pia na wanyama wafugwao ikiwemo mbwa wakati Ziwa Victoria liko jirani na eneo lao.

“Viongozi wetu wametusahau, hebu ona maji ambayo tunatumia ndugu mwandishi, haya maji unayoyaona ndiyo tunayofanyia shughuli zote ikiwemo kunywa, kuoga na kupikia wakati Ziwa Victoria liko hapa jirani,” alisema.

Naye Maganga Mabula, alisema  wanalazimika kuzikana kwenye makazi yao kutokana na kukosa maeneo ya maziko kwa kuwa Serikali imeshindwa kutoa fidia katika maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya makaburi ambapo hivi sasa wanazika nyumbani.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery, aliliambia MTANZANIA kwamba ni kweli kilio cha wananchi hao na kusema suala la makaburi limefikishwa ofisini kwake na tayari jitihada za kulitatua zimeanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles