26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 4, 2024

Contact us: [email protected]

WAFUGAJI WAHOFIA MAPIGANO NA WAKULIMA

Na AMINA OMARI, KILINDI


wafugaji-pxWAFUGAJI walioko Kijiji cha Mswaki, Kata ya Msanja wilayani Kilindi, Mkoa wa Tanga, wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro baina yao na wakulima.

Ombi hilo wamelitoa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo.

Ombi hilo walilitoa baada ya kuwapo kwa tukio la kukamatwa kwa mifugo yao zaidi ya 500 na wakulima kwa kosa la kuingiza mifugo mashambani.

Mmoja wa wafugaji hao, Francis Sosaine, alisema wakulima walichinja ng’ombe wanne wa wafugaji na kujeruhi wengine 17 baada ya kudai kuwa mifugo imeharibu mazao yao.

“Serikali ione namna ya kuingilia kati mgogoro huo kwani umedumu kwa zaidi ya miaka saba sasa bila kupatiwa ufumbuzi wowote.

“Kama hatua za haraka hazitachukuliwa, naamini utafika wakati hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani kila upande unajiona una haki katika uamuzi unaofanyika,” alisema Sosaine.

Naye Lobora Saramba, alisema walinunua visima kwa ajili ya kunywesha mifugo yao, lakini wanashangaa wakulima wamekuwa wakiwavamia mara kwa mara na kuwazuia kwenda kisimani kutumia maji hayo.

“Maeneo yaliyowekwa mifugo yetu tunayamiliki kihalali, lakini tunashangazwa na kitendo cha wakulima kutuzuia kuingiza mifugo na mara kadhaa wanajeruhi mifugo yetu.

“Kwa hiyo, tunaomba hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo kabla hali haijawa mbaya zaidi,” alisema Saramba.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ramadhani Sendege, alikiri kuwapo kwa mgogoro huo na kuomba Serikali ichukue hatua za haraka kumaliza tatizo hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles