23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

WADAU KUKUTANA KUJADILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam


 

jennifer-baarn2ZAIDI ya wadau 300 wa kilimo watakutana kujadili namna ya kuongeza thamani ya mazao na changamoto zinazowapata wakulima wadogo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Mradi wa Ukuzaji Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Centre Limited, Jennifer Baarn, alisem mkutano huo wa mwaka  ambao kauli mbiu yake ni kuibua fursa katika kilimo ‘Unleashing Agricultural Opportunities’, utafanyika Machi 10, mwaka huu katika jengo la LAPF jijini  hapa.

“Kuibuliwa fursa zaidi katika kilimo nchini  kutatanua wigo kwa mazao yote yanayohitaji kuongezewa thamani,” alisema Jennifer.

Alisema katika mkutano huo wa kuongeza thamani, wadau watapata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili kwa kina namna ya kuimarisha kilimo.

“Mkutano huu utawakutanisha maofisa wa Serikali, viongozi wa wakulima, taasisi za fedha na wadau wengine wa kilimo ikiwemo viwanda vinavyotegemea mazao kujiendesha,” alisema.

Alisema kabla ya mkutano huo, Machi 7-8 wadau watafanya ziara ya kutembelea kongani za  Ihemi mkoani Iringa na ile ya Mbarali mkoani Mbeya, kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji inayosimamiwa na SAGCOT.

“Wataona namna mazao kama mchele, soya, nyanya, chai na mifugo inavyosimamiwa kwa lengo la kuongeza thamani. Asilimia kubwa ni wakulima wadogo ambao awali walikuwa wakifanya kilimo kisicho na tija,” alisema Jennifer.

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu huyo alisema kutakuwa na maonyesho ya bidhaa na vifaa vya kilimo ili kudhihirisha namna mradi huu unavyosaidia wakulima wadogo.

Akizungumzia makubaliano ya mkutano uliopita wa tatu, Jennifer alisema walishauri wakulima kuendelea na majukumu yao ili kuongeza tija ya kilimo na vilevile walishauri viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kutoa ushirikiano kwa wakulima ili kuongeza ari na kuondoa vikwazo vitokanavyo na miundombinu au upatikanaji pembejeo za kilimo.

Kwa mujibu wa Jennifer, wadau wataangazia namna taasisi za kifedha zitakavyosaidia wakulima wadogo katika mradi huo na pia uwezekano wa wakulima kujifunza zaidi kuhusiana na kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles