|Hadija Omary, Lindi
Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Ngumbu na Miluwi Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi wamefariki dunia kwa kukanyagwa na tembo wanaodaiwa kutoka katika Hifadhi ya Wanyama ya Msitu wa Selou kwa nyakati tofauti.
Akizungumaza na waandishi wa habari leo Jumanne Agosti 28, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sara Chiwamba amesema siku za hivi karibuni kumekuwa na kundi kubwa la wanyama hao waharibifu kuvamia makazi ya watu na kufanya uharibifu katika mashamba ya wananchi.
“Licha ya tembo hao kuharibu mali za wananchi pia nimepata taarifa kuwa juzi na jan kuna wananchi watatu wamekanyagwa na tembo hadi kuuawa katika kijiji cha Ngumbu na Miluwi hii inatokana na maofisa wahifadhi wetu kufanya kazi vizuri ya kuwatunza wanyama katika msitu huo hali inayosababisha tembo hao kuzaliana kwa wingi na kujikuta wanafika katika makazi ya wananchi,” amesema.