25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WAFANYABIASHARA WANAOTUMIA EFDS WAFIKA 100,000

PATRICIA KIMELEMETA NA CHRISTINA GAULUHANGA

KAMISHINA wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ellijah Mwandumbya, amesema kwa sasa zaidi ya wafanyabiashara 100,015 wanatumia mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs) kwenye biashara zao.

Mwandumbya alisema hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa ukusanyaji wa kodi.

Alisema wafanyabiashara hao ni wale ambao mauzo yao kwa siku yanafika Sh 45,000 na kwa mwaka ni zaidi ya Sh 14,000,000.

“Tuna zaidi ya wafanyabiashara 100,015 wanatumia mashine za EFDs, lengo ni kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato stahiki kulingana na biashara wanazozifanya,” alisema Mwandumbya.

Aliongeza Serikali iliwapa zabuni za usambazaji wa mashine hizo kwa makampuni tisa, hali ambayo imechangia kuwapo kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara kutumia mashine hizo.

Akizungumzia wafanyabiashara wanaodai wamelipa fedha ili kupewa mashine hizo lakini hadi sasa hawajapewa, alisema madai yao yanafanyiwa kazi.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali iko kwenye mchakato wa kufanya tathmini juu ya makampuni yaliyopewa zabuni ya kusambaza mashine hizo kuangalia utendaji wao wa kazi.

“Tathmini hii itafanyika kwa muda wa mwezi mmoja. Tumeanza Agosti, tukimaliza tutaanda ripoti ya kuangalia kampuni iliyofanya vizuri katika usambazaji wa mashine hizo ili tuweze kutoa uamuzi,” alisema.

Alisema mkakati wao ni kuhakikisha ukusanyaji wa kodi unaongezeka, jambo ambalo linaweza kuisaidia Serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles