24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara waanza ‘kupeta’ bandari ya Musoma

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Bandari ya Musoma mkoani Mara, imejidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wafanyabiashara na wadau wa bandari hiyo kwa kukarabati miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa gati la Mwigobero.

Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya wafanyabiashara wamepongeza Jen tihada hizo kwani itaongeza ufanisi na kupunguza gharama za usafirishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Musoma jana, Justine Rukaka ambaye ni Ofisa Uhusiano katika Kiwanda cha kutengeneza  mafuta ya kula yanayotengenezwa kwa mbegu za Pamba cha Mount Meru Millers kilichoko Bunda, amesema Mamlaka ya Bandari Ziwa Victoria imefanya jambo jema kurejesha huduma za usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Musoma kwani huduma hiyo imewaondolea adha ya kusafirisha malighafi na kupunguza gharama za usafiri.

“Awali tulikuwa tunatumia Bandari ya Mwanza ambako ni mbali kulinganisha na Musoma ambako ni karibu hivyo gharama imepungua,” amesema.

Rukaka amesema awali walikuwa wakisafirisha mbegu za Pamba kutoka nchini Uganda na kuzipokelea Bandari ya Mwanza Kusini kabla ya Bandari ya Musoma kurejesha huduma za usafirishaji wa mizigo kwa gharama kubwa.
“Kwa sababu hiyo, tulilazimika mara baada ya kupokea mzigo Mwanza tuusafirishe tena kwa malori kutoka Mwanza kwenda Bunda mahali ambapo kiwanda kipo.

“Tumekuwa tukipokea tani 250 hadi tani 500 za mbegu za pamba kwa mara moja kulingana na ukubwa wa meli inayoleta mzigo siku hiyo, hivyo kwetu sisi imekuwa rahisi kwa uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda kutokana na gharama za usafiri kupungua” amesema Lukaka.

Pamoja na mambo mengine, Rukaka amewaasa wafanyabiashara mbalimbali kutumia bandari ya Musoma kusafirisha mizigo yao ya biashara kwa sababu gharama zake ni za kawaida na unaweza kupakia mzigo kwa wingi tofauti na kusafirisha kwenye malori.

Kwa upande wa Mkuu wa Bandari ya Musoma, Almachius Rwehumbiza amesema bandari hiyo ina uwezo wa kupokea meli tatu kwa wakati mmoja zenye tani 1,500 hari 5,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles