27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa anena mazito Baraza la Eid ElFitr

NA MOHAMMED ULONGO

– TANGA

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaaliwa amewasihi Waislamu na wasiokuwa waislamu waendelee kuishi kwa amani na utulivu huku tukiuenzi mwezi mtukufu uliomalizika jana. 

Majaliwa amegusia kuwa mwezi mtukufu watu huishi kwa amani na busara tele hivyo angependa hali hiyo iendelee kwenye mioyo ya Watanzania wote.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo mkoani Tanga katika Baraza la Eid ElFitr huku akielezea pia kuhusu kampeni ya Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA) ya kudumisha misingi ya elimu ili kusaidia vizazi vya sasa na vya baadae, kwa kuboresha na kujenga shule hapa nchini .

Aidha Majaliwa amefurahishwa na Umoja wa Misikiti mikoani kwa kujenga sehemu za huduma za kijamii kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za jamii hapa nchini.

Katika hotuba yake kwenye Baraza hilo, Majaliwa amewasifia Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini kwa hatua zake za kuboresha miundombinu ya barabara nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, ambako ndiko kuna uhitaji mkubwa wa huduma hizo.

Lakini pia amewataka Waislamu kusahau tofauti zao za kimadhehebu kwani kwa kufanya hivyo wataweza kusukuma mbele Dini ya Uislamu na nchi, kwa kutoa haki ya kila mtu kuabudu dini aipendayo .

Hata hivyo Majaliwa pia amewasihi Waislamu kwenda kupima ili kutambua afya za kila mmoja wao, siyo kutegemea wake zao hasa kuhusu kutambua uwepo wa maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi katika familia.

Sambamba na hilo, amewataka wananchi kukemea vitendo vya rushwa ili kuepuka kudhulumu haki za watu wengine 

Amesema hali ngumu ya kimaisha husababisha vitendo vichafu vya rushwa hivyo anapinga kabisa vitendo hivyo vya rushwa kwa kuwa ni adui wa haki na ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles