26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wafanyabiashara Kagera wampongeza Rais Samia kwa kusamehe kodi ya limbikizo

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera imetoa pongezi za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusamehe limbikizo la kodi ya Huduma (Service Revie) kwa kipindi cha miaka Mitatu.

Kauli hiyo wameitoa juzi mjini Bukoba baada ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan ya siku tatu mkoani Kagera ambapo alihutubia taifa kupitia Mkoa wa Kagera na kutoa msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara iliyokuwa imelimbikizwa kwa miaka mitatu.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kagera, Nicholaus Jovin.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kagera, Nicholaus Jovin amesema kutolewa kwa kauli hiyo kumechochea muitikio kwa wafanyabiashara kufanya biashara pasipo wasiwasi kwani kipindi cha nyuma walikuwa wanakumbana na changamoto nyingi.

Aidha, ameongeza kuwa licha kusamehewa kodi pia imefunguliwa mipaka kwa ajili ya wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera na hata nje ya mkoa kwa kufuata kanununi na sheria zilizowekwa na kusema kuwa pia Jumuiya inampongeza rais kwa kuwaletea Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa kwani ni chanzo cha kukuza uchumi wa mkoa wa Kagera .

Nao wajumbe wa Jumuiya hiyo akiwemo, Richard Maganga amesema kuwa uchumi wa mkoa huo unawategemea Wanakagera wenyewe wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

Pia ameongeza kuwa Jumuiya inampongeza rais kwa kuendelea kuwaondolea vikwazo kuwapatia msamaha wa kodi za malimbikizo za kipindi cha nyuma kwani kabla ya msamaha huo Jumuiya ilikuwa inapitia changamoto nyingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles