27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYABIASHARA 200 WA CHINA KUPIGWA MSASA

NA  FERDNANDA  MBAMILA- DAR ES SALAAM


 

charles-mwijageWAZIRI wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage,  anatarajia kufungua semina itakayowashirikisha wafanyabiashara 200 wa sekta ya ujenzi kutoka China.

Semina hiyo ya siku moja inatarajiwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu na kuhudhuriwa na Balozi wa China nchini.

Habari zinasema  mada zitakazo zungumziwa ni pamoja na mabadiliko ya bajeti ya mwaka  2016-2017.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi  kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), Richard  Kayombo, ilisema semina hiyo itawawezesha wafanyabiashara  wa China kuzingatia na kuzitumia sheria juu ya kutoa kodi sahihi.

Alisema pia itawasaidia kukokotoa kodi  ya uzio katika bidhaa na huduma  na hivyo kuongeza ulipaji wa kodi kwa hiari miongoni mwao.

“Katika semina hiyo mada maalumu zitakazozungumziwa ni pamoja na mabadiliko ya bajeti ya mwaka  2016-2017, masuala ya forodha na uondoshaji wa bidhaa, kodi ya zuio katika sekta ya ujenzi na kodi ya ajira,” alisema Kayombo.

Wafanyabiashara hao watapata  fursa ya  kuuliza maswali  na kupata ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali kuwawezesha kufanya shughuli zao vizuri  kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Pamoja na kuwasaidia katika masuala ya kodi semina hiyo inatarajia kuboresha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles