Gabriel Mushi, Dodoma
Katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) serikali imepanga kupiga kambi kwenye baa na sehemu nyingine za starehe nchini ili kupima wahudhuriaji wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto. Dk. Faustine Ndungulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambale, Masoud Abdalah Salimu (CUF) ambaye alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa ziada kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wa kifua kikuu (TB).
Akijibu swali hilo, Dk. Ndungulile amesema mojawapo ya mikakati ya serikali inayochukuliwa kwa sasa ni kufanya upimaji wa TB kwa Watu wanaoshi na Virusi Vya Ukimwi (Waviu).
“Pamoja na hilo, serikali itaweka kambi katika baa mbalimbali nchini ili kuwapima wateja wa baa hizo Ukimwi hususani wanaume.
“Aidha, serikali inaingiza teknolojia mpya nchini ya upimaji na ugunduzi wa uhakika na haraka wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB),” amesema.