22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

KUBENEA ATAKA WALIOKUMBWA NA BOMOA BOMOA KIMARA WALIPWE

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea (Chadema) ameitaka serikali kuwalipia fidia wakazi wa Kimara waliokumbwa na bomoa bomoa kupisha upanuzi wa barabara kuu ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kiluvya.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano ambapo pamoja na mambo mengine amesea Benki ya Dunia ambayo ni mfadhili wa mradi huo imesitisha kutoa fedha kwa sababu wananchi hao hawajalipwa fidia.

Amesema ubomoaji wa nyumba hizo zilizo ndani ya mita 121.5 kutoka katikatika ya barabara ulifanyika kinyume cha sheria ya barabara.

“Namuomba waziri kwa kuwa tayari nyumba za wananchi wa Dar es Salaam zimevunjwa na Benki ya Dunia imesimamisha msaada kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kuwa ujenzi umekiuka taratibu na kukiuka haki za binadamu, serikali iwafidia wananchu wa ubungo ambao nyumba zao zimevunjwa  bila kufanya tathmini ya kile kilichovunjwa.

“Watalaamu wanasema ukubwa wa eneo hilo ambalo limetwaliwa na Wakala wa Barabara (Tanroads), lina upana sawa na ukubwa wa viwanja viwili vya mpira, hili ni jambo ambalo halipo katika ujenzi wa barabara,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Kubenea amesema serikali italazimika kulipa fidia ili mradi uendelee lakini hajui italipaje ilihali tayari nyumba zimenjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles