28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wade ajiunga na Chicago Bulls

Dwyane Wade
Dwyane Wade

CHICAGO, MAREKANI

NYOTA wa mchezo wa kikapu, Dwyane Wade, amejiunga na timu ya Chicago Bulls baada ya kuitumikia Miami Heat kwa misimu 13.

Wade mwenye umri wa miaka 34, anatarajia kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atasaini kwa kitita cha pauni milioni 36.2 sawa na dola milioni 47.

Kwa kipindi cha misimu 13, mchezaji huyo aliisaidia timu yake ya Miami Heat kuchukua mataji matatu ya Ligi ya NBA, huku akiitwa kwenye kikosi cha All Stars mara 12.

Juzi usiku mchezaji huyo aliwaaga mashabiki wa timu hiyo ya Miami na kuwashukuru kwa ushirikiano wao ambao waliuonesha kwa kipindi chote.

“Nimekuwa hapa kwa kipindi kirefu, nimejifunza mengi, lakini sasa ni wakati wangu wa kubadilisha mazingira, ila ninaushukuru uongozi wa Miami na mashabiki kwa ujumla kutokana na ushirikiano wenu kwangu, sasa natarajia kujiunga na Chicago, ila nitabaki nawapenda,” alisema Wade.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles