Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam
Wadau wa mpira wa Miguu kigamboni wametakiwa kujitokeza kuthibitisha ushiriki wa Mafunzo ya ukocha ngazi ya awali yaliyopangwa kuanza Machi 6 hadi 15 mwaka huu kwenye Ukumbi wa CCM Kigamboni, Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Kigamboni(KDFA) kwa kushirikiana na Chama cha Makocha (TAFCA) wilayani hapa.
Akizungumza na www.mtanzania.co.tz ,Katibu Mkuu wa KDFA, Lawrence Ngauga,amesema uthibitisho huo utaenda sambamba ulipaji wa ada Sh 100,000 sare Sh 10,000 na cheti Sh 10,000.
Amesema milango bado ipo wazi kwa washiriki kujitokeza kwa wingi kujisajili ushiriki wao.
“Tayari washiriki 20 wamejitokeza hadi sasa na tunahitaji 10 ili kutimiza idadi ya washiriki 30 watakaofaidika na mafunzo haya,” amesema Ngauga.
Ngauga ameongeza kuwa lengo ni kuwajengea uwezo walimu wa mpira na wawe na taalum ya kusaidia kuinua na kuinua vipaji ndani na nje ya wilaya