25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa mbegu nchini waiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria

Na Christina Gauluhanga, Mtanzania Digital

WADAU wa mbegu nchini wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria ya mbegu ya mwaka 2010/2014 ili kuondoa mapungufu yaliyopo kwa sasa.

Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma wakati wadau wa kilimo zaidi ya 300 walipokutana na kuchangia namna bora ya kuendeleza kilimo Hai wakati wa Mkutano wa PIli wa Kilimo Hai Kitaifa, ulioandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Ufaransa,Umoja wa Ulaya EU),Shirika la Umoja wa mataifa la Chakula (WFP) na wengineo.

Akizungumzia kuhusu sheria ya mbegu na ubora wake, Mkurugenzi wa Asasi inayoshughulika kuendeleza kilimo Hai (IMITRA), Deusdedit Kizito amesema sheria iliyopo sasa inahitaji maboresho ili kuendana na wakati wa sasa ambapo mazao ya kilimo hai yamekuwa na soko kubwa.

Amesema ni muhumu kuwa na tamko la wazi ambalo litakuwa na sera ya kitaifa itakayohusu mbegu.

Ameongeza kuwa ni wakati sasa wa Wizara husika kupitia Halmashauri kuelekeza kutungwa kwa kanuni ngazi ya kata ambazo zitasaidia ufuatiliaji na upatikanaji wa mbegu bora za asili na kuzihifadhi pamoja.

“Ni vema mchakato ukaanzia ngazi ya Halmashauri ili kuweza kuwasajili wakulima na kuwatambua kwakuwa itasaidia kuwapa elimu pamoja na kuwatafutia masoko ya uhakika,” amesema Kizito.

Amesema kumekuwa na changamoto ya mwingiliano wa mbegu za asili na za kisasa hali inayosababishaa upatikanaji wa mazao chotara.

” Kongamano hili la Pili la Kilimo Hai litasaidia wakulima kuhifadhi mbegu za asili zilizo bora, kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo na kupata masoko ya uhakika,” amesema Kizito.

Amesema msingi wa kilimo hai ndio msingi mkuu wa afya ya jamii hivyo ni muhimu kujadili changamoto zilizopo ili kuondoa sehemu ya mabaki ya viwatilifu yanayojitokeza kwenye baadhi ya mazao hayo.

Amesema hadi sasa wakulima 600 nchini wanalima kilimo hai ni vema wakathibitishwa ili kuendeleza kilimo hai na kuzalisha chakula cha kutosha nchini.

” Tunaiomba Serikali ikaanzisha utafiti wa kina kuhusu mbegu na jinsi ya kuzihifadhi mbegu ili zisishambuliwe na wadudu,” amesema.

Pia wameomba kuwe na taarifa ya pamoja ya kilimo Hai Kitaifa ambayo itaelezea tafiti mbalimbali.

Kizito amesema suala la mbegu ni la mtambuka lisihusishe Bara na Visiwani pekee bali liwe la nchi nzima.

Amesema ni muhimu kuwa na tamko la wazi ambalo litakuwa na sera ya kitaifa kuhusu mbegu.

“Hata hawa wa visiwani wana mashamba huku Bara na tumekuwa tukiepeana mbegu hivyo ni muhimu kuwa na tamko tu la pamoja,” amesemw Kizito.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza kilimo Hai SAT, Janeth Maro ameiomba Serikali ipunguze gharama za uthibitishaji bidhaa kwakuwa ipo juu na inachangia wakulima wengi kushindwa kumudu.

Amesema endapo gharama zitapungua itasaidia wakulima wanaokidhi viwango kuthibitisha bidhaa zao.

Pia aliomba serikali iwasaidie kuwepo na usalama wa uwekezaji ndani na nje ili kulinda mitaji ya wawekezaji.

Alisisitiza umuhimu wa uwepo pia wa masoko ya uhakika wa mazao ya kilimo hai ili kumlinda mkulima na mlaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles