25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Fedha za IMF siyo za kulipana posho-Ndalichako

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewatahadharisha kuwa fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hazihusishi ulipanaji wa posho ya aina yoyote na viongozi wa taasisi zinazohusika na kwamba yeye atafuatilia kwa ukaribu katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Pia, ametoa maelekezo kwa watendaji wa wizara pamoja na taasisi zitakazotekeleza miradi wahakikishe maandalizi ya mpango wa matumizi ya fedha hizo yanakamilika ndani ya Oktoba 30, mwaka huu sambamba na kutoa mpango wa utekelezaji wa miradi itakavyofanyika.

Maagizo hayo ameyatoa leo Oktoba 23, 2021 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari, wakati akitoa taarifa huhusu utekelezaji wa mpango wa  maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Waziri Ndalichako amewatahadharisha kuwa fedha zilizotolewa na  IMF hazihusishi ulipanaji wa posho ya aina yoyote na viongozi wa taasisi zinazohusika na kwamba yeye atafuatilia kwa ukaribu katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Nitafuatilia kwa karibu kuhakikisha maagizo ya Mheshimiwa Rais kuhusu matumizi sahihi ya fedha hizo yanatekelezwa kikamilifu.Nawapa tahadhari watumishi wote wa Wizara wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huu kuwa nitakuwa makini katika kuhakikisha kuwa mpango huu unatekelezwa kwa ufanisi kuanzia hatua ya maandalizi hadi utakapokamilika kwa wakati uliopangwa,”amesema 

Amesema kuwa  sekta ya Elimu imetengewa bilioni 368.9 na Wizara ya Elimu imepata Sh bilioni 64.9 kutekeleza miradi iliyochini ya wizara hiyo.

Amesema kuwa hadi ifikapo Oktoba 30, 2021 kila taasisi itakayotekeleza mradi huo iwe imekamilisha maandalizi na mipango ya utekelezaji pamoja na kuandaa mpango kazi utakao ainisha hatua mbalimbali za taratibu za manunuzi ya huduma na vifaa.

“Hadi tarehe 30 mwezi huu kila taasisi iwe imekamilisha na iainishe lini vifaa vitanunuliwa, vifaa vyote vinunuliwe kwa kuzingatia bei ya soko nataka na mimi nikienda kununua kifaa bei iwe ndio hiyo,” amesema Prof. Ndalichako.

Waziri huyo ameagiza miradi hiyo kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo May 30, 2022 na kusisitiza matokeo ya utekelezaji wa mradi yaendane na thamani ya fedha zilizotolewa na si vinginevyo.

“Namuagiza Katibu Mkuu wa Wizara aandae mfumo wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi utakaowezesha kubaini changamoto zitakazo kuwa zikijitokeza na kuchukua hatua stahiki na kwa wakati” amesema.

Prof Ndalichako amezema fedha hizo zitakwenda kuimarisha ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo shilingi bilioni 1.47 zimetengwa, kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 57.98 zimetengwa na kuimarisha mazingira ya utoaji elimu ya ualimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles