23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa Madini, Biashara Kilimanjaro kumuenzi Magufuli

Na Upendo Mosha,Rombo

Wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda na biashara, mkoani Kilimanjaro, wamesema watamkumbuka Hayati Dk. John Magufuli na kwamba wataenzi sekta hiyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Akizunguza na Waandishi wa Habari jana Mwekezaji wa Kampuni ya Bella View inayojihusisha na uzalishaji wa maji safi na juisi wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, Shanel Ngowi, alisema taifa limepata pigo kubwa la kuondokewa na Hayati Dk.Magufuli.

Mwekezaji wa Kampuni ya Bella View, Shanel Ngowi.

Alisema katika kuenzi yale yote mazuri yaliokuwa yakifanywa na Hayati Dk.Magufuli wawekezaji na wafanyabiashara wanawajibu mkubwa wa kumuenzi kwa vitendo ikiwemo kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kutegemea uchumi wa viwanda.

“Hayati Dk. Magufuli alikuwa akituimiza kufanya uwekezaji katika sekta ya viwanda tunaahidi tutayaenzi yale yote ambayo yalikuwa ni maono yake maana alikuwa na maono mkubwa sana..msiba huu ni mzito lakini lazima yukabiliane nalo,kila kundi na kila sekta marehemu aliaacha alama tumuenzi kwa hayo”alisema Ngowi

Alisema katika utawala wake wa miaka mitano,sekta ya viwanda inajivunia kupatikana kwa umeme wa uhakika jambo lililowasaidia wawekezaji kufanya uzalishaji wa uhakika ambao umesaiia kuleta ushindani katika soko la Afrika Mashariki.

Alisema Hayati Magufuli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa ukiritimba katika sekta mbalimbali ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji jambo ambalo lilisaidia kupandisha uchumi wa nchi na kufikia uchumi wa kati.

“Katika utawala wake alijitahidi kurudisha nidhamu katika idara mbalimbali za serikali na kusababisha viwanda vingi kuengwa na hatuwezi kumsahau kwasababu alilinda soko la bidhaa zetu za ndani haswa kwa sisi wazalishaji wa maji,”alisema

Akimzungumzia Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, alimpongeza na kwamba wawekezaji wanaimani mkubwa naye katika kuboresha sekta ya viwanda kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji jambo ambalo litawavutia zaidi wakezaji kuwekeza.

“Nampongeza Mama Samia kwa kuwa Rais wa Tanzania, tunaimani naye na tunajua anafahamu changamoto za wawekezaji, tunahitaji kusikilizwa ni kwa jinsi gani tunaweza kuondolewa kodi ambazo sio rafiki jambo hili litatusaidia kukua na bidhaa zetu kuwa na ushindani sokoni,” alisema

Naye Mfanyabishara katika Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, alisema kifo hicho ni pigo kwa taifa na kwamba watamkumbuka katika kusimamia misingi bora ya ufanyaji wa biashara pamoja na kuigania maslahi ya wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles