28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Matukio katika picha: Ibada maalum ya mazishi ya Hayati Dk. Magufuli

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge, wasanii pamoja na wananchi tayari wamefika katika uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita tayari kwa ajili ya ibada maalum ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Magufuli.

Viongozi mbalimbali,wasanii na wananchi walianza kuingia katika viwanja vya Magufuli kuanzia majira ya saa 11 alfajiri tayari kabisa kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Pombe Magufuli.

Stanslaus Mabula mbunge wa jimbo la Nyamagana ni miongoni mwa wabunge waliofika Chato katika viwanja vya Magufuli kwaajili ya kumshiriki misa maalum ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Magufuli.

Mwili wa Hayati Magufuli umefika katika viwanja vya Magufuli majira ya saa 03:45 asubuhi na kupokelwa kwa Majozi makubwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge, wasanii pamoja na wananchi waliofika katika uwanja huo wa Magufuli.

Hayati Magufuli anatarajiwa kuzikwa leo wilayani Chato baada ya Ibada maalumu na Salamu mbalimbali kutolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles