28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa dhahabu waomba kibano zaidi utoroshwaji madini hayo

Na Saimoni Mghendi-Kahama

WAFANYABIASHARA wa dhahabu na madalali (Broker), wanunuzi wadogo wadogo (kota) na wanunuazi na wauzaji wakubwa (dealer), wameiyomba Serekali  kuongeza nguvu ya udhibiti wa utoroshwaji wa madini hayo hasa kwenye machimbo.

Ombi hilo limetolewa na wadau hao jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika soko kuu la madini la Mkoa wa Kahama.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wengine wa madini ya dhahabu Renatus Maji, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Soko la Madini Kahama, alisema bei ya soko ni nzuri, dhahabu imepanda bei ukilinganisha na siku za nyuma ambapo mipaka ilikuwa imefungwa kwa sababu ya corona.

“Dhahabu imepungua sokoni na niwaombe Serikali waongeze bidii kudhibiti hasa kwenye masoko holela ya machimboni ambapo huko huuzwa dhahabu nyingi kuliko huku kwenye soko rasimi” alisema Maji.

Maji aliiomba Serikali kuwatambua Makota na Broka kwa kuwatengenezea vitambulisho kama vya machinga  watambulike na Serekali wafanye kazi kwa uhuru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Shinyanga, Alphonce Paul, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kupunguza msururu wa kodi kwenye madini.

“Tulipotoa maoni yeye alituskia na akafuta kodi zilizokua kandamizi, pia amewatambua wachimbaji wadogo na kuwapa leseni, amefungua mipaka na kufanya hali ya soko sasa kuwa nzuri jambo ambalo sisi tunaona faida,” alisema Paul.

Naye mdau wa madini ya dhahabu, Emanuel Kidenya, alisema toka mipaka imefunguliwa baada ya corona kuisha, faida ya dhahabu imeongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles