24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC aonya vyama vya msingi kuwaibia wakulima

Na DERICK MILTON-SIMIYU

MKUU wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, amesema wakati msimu wa ununuzi wa pamba 2019/20 ukiendelea katika mikoa inayozalisha zao hilo, kumedaiwa kuika kwa wizi mpya kwenye malipo ya wakulima wa zao.

Alisema hali hiyo imetokea katika kipindi cha wiki moja tangu makampuni ya ununuzi wa zao hilo, kuongeza bei ya pamba kutoka bei elekezi ya Serikali Sh 810 hadi kufikia Sh 900.

Ongezeko hilo la bei limetokana na uhitaji mkubwa wa pamba, huku uzalishaji ukiwa mdogo katika msimu huu, hali iliyofanya wanunuzi kushindana kwenye bei.

Kiswaga akizungumza wenyeviti na makatibu wa Vyama vya Msingi (AMCOS) Wilaya ya Bariadi, Kiswaga alisema wizi huo unaofanywa na vyama hivyo ni mpya.

Alisema tangu ongezeko la bei ya pamba lianze, wakulima wamekuwa hawalipwi nyongeza hiyo kwa baadhi ya maeneo, badala yake wanalipwa Sh. 810 ambayo ni bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.

Alisema viongozi wa Amcos wamekuwa wakichukua nyongeza hiyo kwa madai kuwa inatakiwa kwenda kwenye chama kwa ajili ya wao kujilipa posho huku mkulima wakimlipa bei elekezi.

“ Yapo makampuni yananunua pamba kwa Sh 830, mengine Sh 850 hadi Sh 900, kutoka bei elekezi ya Sh 810, tumegundua zipo Amcos viongozi wake wanachukua fedha zilizozidi kwenye bei elekezi na kuwapa wakulima Sh 810.

“Kama kampuni ikinunua pamba kwa Sh. 850 kwa kilo moja au Sh 900, hiyo Sh 40 au Sh 90 wanachukua watu wa Amcos na wakulima,” alidai Kiswaga.

Alisema wameanza kufuatilia viongozi ambao wanafanya hivyo, na watakaobainika hatua kali dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika uongozi.

Alisema ongezeko hilo linatakiwa kumnufaisha mkulima mwenyewe na siyo viongozi wa Amcos, na wala hakuna maelekezo ya Serikali ambayo yamewataka wachukua nyongeza hiyo.

Alisema bei kama imeongezeka mkulima anatakiwa kulipwa kiasi chote cha pesa na siyo kumkata, ambapo aliwataka wanunuzi wote mkoani humo kuweka mabango ya bei zao katika kila Amcos ambako wananunua pamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles