22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

WADAU UTALII WAMLILIA MMILIKI IMPALA HOTELS

Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA

CHAMA cha Wakala wa Utalii Tanzania (Tato) kimesema kifo cha mmiliki wa Hoteli za Utalii za Impala, Naura Springs na Ngurdoto za jijini hapa, Faustine Mrema, ni pigo katika sekta ya utalii.

Kimesema Mrema alikuwa mtu muhimu katika sekta hiyo kwa kuwa alikuwa amewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA   jana, Katibu Mtendaji Mkuu wa Tato, Sirili Akko, alisema kifo cha Mrema kimeacha pengo katika sekta ya utalii kwa kuwa enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa wa kuiendeleza sekta hiyo.

“Ninasikitika kutokana na kifo cha mdau huyu wa utalii, sekta yetu imepata pigo kutokana na kifo chake.

“Mbali na kumiliki hoteli, pia alikuwa anamiliki kampuni ya utalii inayosafirisha watalii. Kwa hiyo  utaona ni kwa jinsi gani alivyotoa mchango kwa jamii kutokana na ajira zilizozalishwa na makampuni yake,” alisema Akko.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu Mrema, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelism Tanzania, Dk. Eliud Issangya, alisema kifo cha Mrema kimeacha simanzi katika jamii kutokana na mchango alioutoa.

“Mrema nilifahamiana naye mwanzoni mwa miaka ya 1980 wakati huo mimi ndiyo naanza kazi hii ya uchungaji.

“Yeye wakati huo alikuwa anaanza biashara ya kufua nguo kama dobi akiwa na mashine ndogo. Nilikuwa nampelekea nguo zangu afue, ndiyo tukajenga urafiki wa karibu uliodumu mpaka leo kiasi kwamba alikuwa si tu rafiki bali ndugu yangu na mwanafamilia,” alisema Dk. Issangya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles