27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

WADAU HAKI ZA BINADAMU WAITAKA MAHAKAMA KUMPA DHAMANA NONDO

Na Asha Bani, Dar es Salaam


Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) kwa kushirikiana, Mtandao Wa Wanafunzi (TSNP) na Kituo cha Haki za Binamu wamepeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kuitaka itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumpeleka Abdul Nondo Mahakamani au kumpa dhamana wakati shauri la msingi likiwa linaendelea.

Onesmo Olengurumwa Mratibu Wa mtandao wa THRDC, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kijana huyo anashikiliwa kwa siku nane bila hata ndugu, jamaa na wanafunzi wenzake kujua alipo.

“Kimsingi ananyimwa haki ya kikatiba ya kuzungumza kile kilichomkuta, wakati Jeshi la Polisi tayari limeshatoa taarifa,” amesema.

Naye Katibu wa TSNP, Joseph Malekela amesema ni jambo la kushangaza kuona mwenzao anashikiliwa hadi leo bila hatua zozote kuchukuliwa.

“Tumezunguka vituo vyote bila mafanikio, hatujui yuko wapi, tunajibiwa na wakuu wa vituo hawajui, hawajui ni jambo la ajabu wakati mzazi wake akiwa mgonjwa mkoani Kigoma yanatukia haya,” amesema.

Kwa mujibu wa wanafunzi hao baba wa Nondo amewaomba wamsaidie katika kutafuta haki ya mwanawe ikiwamo kujua alipo kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles