26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

WACHIMBAJI WALALAMIKIA KERO YA MAJI MGODINI

 

 

Na Odace Rwimo,

WACHIMBAJI wa dhahabu katika mgodi wa Kitunda  wilayani Sikonge   wamelalamikia kero ya maji   katika mgodi huo.

Kwa mujibu wa wachimbaji hao,  hali hiyo inafanya shughuli za uchimbaji na usafishaji dhahabu kutofanyika kwa ufanisi.

Walikuwa wakizungumza  na waandishi wa habari waliotembelea mgodi huo juzi.

Hali ya maji ni mbaya kwa sababu  dumu moja   la lita 20 wanauziwa Sh 1000 na kwa siku wanaweza kutumia madumu matano  hadi 10 na yanapatikana umbali mrefu sana, walisema.

Walisema shughuli za uchimbaji madini zinahitaji maji mengi   kila siku lakini hakuna chanzo chochote cha maji katika eneo hilo.

“Tunaomba serikali itusaidie kupata maji ya uhakika katika mgodi huu  ikiwezekana maji ya bwawa la Igumila lililoko Kitunda takribani umbali wa km 22 yaweze kuvutwa na kufikishwa hapo,”  alisema Salum Songwe mchimbaji kutoka Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Mama Christina, mtoa mama ntilie kutoka Nyakato, Mwanza, alisema wanapata shida kubwa  kupika chakula kutokana na uhaba wa maji   katika mgodi huo hali ya usafi hairidhishi kwa kero hiyo.

Alisema kwa hali ilivyo wachimbaji wanaweza kukaa hata mwezi mzima bila kuoga au kufua nguo zao.

Alisema  jambo hilo linahatarisha usalama wa afya zao achilia mbali ufanisi wa kazi yenyewe ya kusafisha mchanga wa dhahabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles