24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji, viongozi kikapu watakiwa kuchanja

Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania( TBF), Phares Magesa amewataka viongozi wa klabu mbalimbali zitakazoshiriki michuano ya Kimataifa ikiwamo  ya BAL na FIBA Afrika ‘Club Championships Tournaments’, kuhakikisha wanapata chanjo ya Uviko -19 ili kuepuka usumbufu.

Magesa amesema leo, huku akiziorodhesha timu ambazo wachezaji wake wanatakiwa kuchanjwa mapema ambazo ni Kurasini Heats, JKT Stars na Donbosco Lioness.

Aidha, Magesa amesema timu ambayo haitatekeleza hayo haitaruhusiwa kushiriki mashindano ya hayo hivyo ni vema wakaepuka usumbufu usio wa lazima.

Wakati huo huo, timu za mikoa mbalimbali zinaendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mashindano ya kikapu maarufu kama CRDB Bank Taifa Cup, yatakayofanyika mwezi ujao, Chinangalu, jijini Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles