NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM
UTARATIBU wa klabu kuteua wachezaji kuwa makocha katika timu walizocheza ni  jambo linaloonekana kuongeza uzuri wa mchezo wa soka duniani.
Ni utamaduni ambao haukuwa maarufu kabla ila umeonekana kuchukua nafasi kubwa kwa siku za karibuni, Â kwa kuwa klabu inaamini kwamba kocha bora lazima awe na ufahamu kuhusu tamaduni ya klabu husika, ajue namna ya kuwasiliana na wachezaji pamoja na viongozi na ushawishi wa mafanikio.
Hiyo ndio sababu ya klabu kuamua kuteua wachezaji ambao walikuwa wenye mafanikio katika timu ambao kupitia rekodi zao wamekuwa na ushawishi wa kiuongozi katika benchi la ufundi la timu hiyo.
Wafuatao makocha 10 ambao waliwahi kuzifundisha timu walizocheza na baadae kuhamia kwingine.
- Senol Gunes
Senol Gunes ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Besiktas ya Uturuki aliwahi kucheza nafasi ya kipa akiwa timu ya Sebat Genclik, Trabzonspor na timu ya taifa ya Uturuki.
Kocha huyo aliwahi kuitumikia Trabzonspor, kwa miaka 15, Gunes aliiongoza timu yake ya zamani kwa maika mine hadi mwaka  2013 alipojiunga na Besiktas.
- Massimo Carrera
Massimo Carrera (53), aliwahi kuwa beki wa kati wa timu ya Juventus, Napoli na Italia kwa vipindi tofauti.
Kwa sasa Carrera anaifundisha timu ya Spartak Moscow ya Urusi kwa mara ya kwanza akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Dmitri Alenichev baada ya kuwa kocha msaidizi akiwa Juventus na  timu ya taifa ya Italia.
- Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino aliwahi kucheza katika timu za Espanyol, PSG na timu ya taifa ya Argentina
Mchezaji ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Tottenham Hotspur kwa miaka mitatu aliyoifundisha timu hiyo amefanikiwa kuiongezea thamani kwa kuipandasha hadi katika timu nne bora katika msimamo wa Ligi Kuu England.
Katika kipindi chake wakati akicheza timu ya taifa ya  Argentina alibaki kuwa shujaa katika timu ya Espanyol, baada ya kutumia miaka nane Ligi Kuu La Liga kabla ya kuwa kocha kwa mara yake ya kwanza.
- Darko Milanic
Milanic alikuwa akicheza nafasi ya beki wa kati katika timu ya Partizan Belgrade, Sturm Graz na timu ya taifa ya Slovenia
Nahodha huyo wa Slovenia katika michuano ya Euro ya mwaka 2000 kwa sasa anaifundisha timu ya Maribor ambayo mwaka jana ilifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kocha huyo aliwahi kuifundisha timu ya Leeds United mwaka 2014 na kuwa kocha wa kwanza ambaye hakuwa Muingereza kuifundisha timu hiyo.
- Sergio Conceicao
Mreno Sergio Conceicao amewahi kucheza katika timu za C Porto, Inter Milan na timu ya taifa ya  Portugal.
Kwa sasa anaifundisha timu ya FC Porto ambayo akiwa mchezaji alikuwa akicheza nafasi ya winga wa kulia katika mfumo wa 3-5-1-1 ambao anaendelea nao hadi sasa.
Kocha huyo ambaye alifanya vizuri akiwa kocha wa Lazio ambako alisaini miaka miwili na baadae kuhamia Nande kwa mkataba wa mwaka mmoja kabla ya kuhamia FC Porto.
- Giovanni van Bronckhorst
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Netherlands, Bronckhorst kwa sasa anaifundisha, Feyenoord
Van Bronckhorst alikuwa nahodha wa Netherland katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2010.
Nyota huyo pia nalikuwa nahodha wa timu ya taifa katika michuano mikubwa sita akiwa na mafanikio makubwa katika LIgi Kuu England na La Liga.
- Diego Simeone
Simeona amewahi kuwa mchezaji wa  Inter Milan, Lazio na timu ya taifa ya  Argentina kabla ya kuifundisha Atletico Madrid.
Huyu ni miongoni mwa makocha bora duniani ambaye aliwahi kucheza Atletico Madrid misimu miwili kabla ya kuifundisha tangu mwaka 2011.
Ni miaka sita sasa tangu awe kocha mkuu, amefanikiwa kuiweka katika ramani ya klabu bora duniani akifanikiwa kutwaa taji la La Liga mwaka 2014 na kuingia mara kadhaa katika fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.
- Pep Guardiola
Guardiola ni mwamba mwingine katika soka ambaye kabla ya kufundisha alikuwa mchezaji wa Barcelona, Roma na timu ya taifa ya Hispania.
Kocha huyu ambaye alikuwa akicheza nafasi ya kiungo kwa sasa anaifundisha timu ya Manchester City anaonekana kuwa matamanio makubwa ya kuendelea kuwa bora Ulaya akiwa na timu hiyo.
Akiwa mchezaji alishinda mataji sita ya  La Liga huku mawili akiwa nahodha akiwa Barcelona.
- Antonio Conte
KIU NGO wa zamani wa Lecce, Juventus na timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte kwa sasa hana timu anayoifundisha baada ya kutemwa na Chelsea.
Conte limekuwa jina kubwa katika makocha bora barani Ulaya, mafanikio yake yamekuja baada ya kuitumikia Juventus kwa miaka 13Â akishinda mataji manne ya Serie A na Ligi ya Mbingwa Ulaya.
- Zinedine Zidane
Kwa sasa ukitaja jina la Zidane, mashabiki wa Real Madrid wanakumbuka mambo mengi mazuri kuhusu yeye.
Mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamemfanya kuwa na soko kubwa kwa klabu za Ulaya ikiwamo Manchester United inayomuhitaji kwa sasa.
Kocha huyu aliwahi kucheza timu ya Juventus, Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kuwa kocha wa timu ya vijana ya Real Madrid na baadae kupandishwa hadi ya wakubwa ambako ndiko alipopata mafanikio makubwa katika mchezo wa soka baada ya kutundika daluga.