24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

EDDIE MURPHY ATARAJIA MTOTO WA 10

NEW YORK, MAREKANI


MCHEKESHAJI maarufu nchini Marekani, Eddie Murphy, ametangaza anatarajia mtoto wake wa 10 siku za hivi karibuni.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 57, amedai baada ya kufanya vipimo na mke wake, Paige Butcher, wamegundua kuwa mtoto huyo ni wakiume na wanamtarajia kumpata Desemba mwaka huu.

Hata hivyo, mtoto huyo atakuwa wa pili kwa wawili hao tangu walipofunga ndoa 2012, lakini watoto wengine nane aliwapata kwa mama wengine.

“Nina furaha kuona napata mtoto mwingine wa kiume, wote kwa ujumla tuna furaha, hivyo familia inazidi kuwa kubwa kama tulivyopanga,” alisema msanii huyo. Mtoto wa kwanza wa wawili hao walimpata tangu Mei 2016 na kumpa jina la Izzy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles