27.1 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wachepushaji sugu wa maji mto Ruvu watiwa mbaroni

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ukaguzi uliofanywa na Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu katika maeneo tofauti tofauti ya vyanzo vya Maji kwa lengo la kuwaondosha na kuwapa elimu Wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya Maji kinyume na kifungu cha 64(1)(a-c) cha sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji , Sura ya 331.

Katika ukaguzi huo umefanikiwa kukamata Pampu tatu za kusukuma maji ambazo hutumika kuchepusha maji kutoka Mto Ruvu unaotegemewa na wakazi wa jijini Dar es Salaam na Pwani jambo ambalo husababisha kupungua kwa wingi wa maji.

Wananchi hao waliopo katika kijiji cha Madege kata ya Duthumi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani hutumia Pampu za kusukuma Maji katika mashamba yao pamoja na kuuuza kwa wanachi wengine bila ya kuwa na Kibali cha matumizi ya Maji kinachotolewa na bonde la Wami/Ruvu.

Katika operesheni hiyo mtu mwingine alikamatwa akitumia Pampu kuchepusha maji na kuleta katika eneo ambalo hutumia kuoshea magari katika kijiji cha Msolwa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze.

Wakati huohuo katika operesheni iliyofanyika Vitongoji vya Kihumbageni na Kisaki kituoni bodi imefanikiwa kukamata Pampu nne za Kusukuma Maji, wafugaji Watatu waliokuwa wamepeleka Ng’ombe katika vyanzo vya maji na mkulima mmoja aliyekuwa hana kibali cha matumizi ya maji kutoka bonde la Wami/Ruvu

Kikosi kazi Kiliweza kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji kwa viongozi wa vijiji ili viongozi waweze kufikisha elimu kwa wananchi wao kufuata kanuni, taratibu na sheria ya matumizi ya maji.

Kiongozi wa operesheni kutoka bonde la Wami/Ruvu, Mshuda Wilson amesema kuwa ni vyema Wananchi kufuata maagizo yanayotolewa na Bodi kwa matumizi ya maji kama kuomba vibali kwani vibali vinapatikana wafuate utaratibu wa kuvipata. Watu wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yao na wengine kulipa faini.

Shuhuda ameongeza kuwa Wananchi kuwa rafiki kwa kushirikiana na Taasisi ya Wami/Ruvu katika kutunza na kuhifadhi Vyanzo vya Maji kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu na kuwaomba Wananchi wasamaria kuendelea kutoa taarifa juu ya wavamizi na waharibifu katika Vyanzo vya Maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles